Hicho kilichopo hapo ni sahihi sibishani nacho.
Lakini kumbuka Kijana usipendelee kujifunza kila Kitu kupitia Google hasa Wikipedia kwani hata mimi na Watanzania wengi tunazo valid account za Wikipedia tunatupia tu mizigo huko utabeba Pumba huko uje uuumbuke.
Ndugu Wikipedia haipost Vitu wenyewe na wala wanaopost habari zao haziwi verified hivyo ni Shamba la Bibi kila Mtu anajiandikia huko.
Kama kweli na wewe unataka kujifunza Sheria za Soccer basi tafuta Kitabu kinachoitwa "LAWS OF GAME" ni cha FIFA wenyewe ndiyo humo utazipata Sheria zote 17 za Soccer.
Kama unahitaji Softcopy nitumie email yako Inbox nitakutumia ili usome Sheria halisi za Soccer uepukane na hizi Aibu ndogondogo.