Wadau wa Sportbikes, siku ukitaka kufanya maamuzi magumu ifikirie na Ducati Panigale V4

Wadau wa Sportbikes, siku ukitaka kufanya maamuzi magumu ifikirie na Ducati Panigale V4

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Ducati ni kampuni la kutengeneza pikipiki kutoka Italy, na ni ndugu wa damu na Lamborghini ambae ni mmiliki, na wote mzazi wao akiwa ni Audi na Babu yao ni Volkswagen Group.
Ducati_Panigale_V4_-_Tuning_World_Bodensee_2018,_Friedrichshafen_(OW1A0484).jpg

Sasa Ducati ni wababe sana kwenye ulimwengu wa Sportbikes na Superbikes, wale wapenzi wa MotorGP watakua mashahidi. Jamaa wamekua wakitengeneza powerful bikes miaka nenda miaka rudi.

Sasa pamoja na kua na series nyingi huko nyuma, mwaka 2018 waliitroduce hii Panigale V4. Hii series ina versions mbalimbali ila inayovutia zaidi ni hii Panigale V4.
Ducati_Panigale_V4_R_(2).jpg

Hii chuma Panigale V4 ina engine ya cc 1,100 ikiwa na 4 cylinders katika layout ya V. Engine ina uwezo wa kutoa hadi 200+ hp kutegemea na version na zinaweza kufika hadi max speed ya 370 km/h.
Ducati_Superleggera_V4_-_container.jpg

Bei kidogo sio rafiki, mpya ni takribani $35,000/= ila inaweza kushuka chini ukipata used ya miaka ya 2018 hadi 2020.

Tukutane Bagamoyo trip.
 
Aisee SI itakua inapaa, hawa bodaboda wa kichina wakiendesha speed 60 nawaomba wapunguze mwendo so huyo akifika 200 inakuaje?
 
Mjini Mzizima mbona watu wanayo matoleo ya nyuma.

Kwenye Bike Honda ndio mbabe wa muda wote
 
Mjini Mzizima mbona watu wanayo matoleo ya nyuma.

Kwenye Bike Honda ndio mbabe wa muda wote
Hizo ndizo zilizo kwenye soko, zinajulikana na wengi ila US wana kampuni inaitwa Harley davidson ni balaa hatuzioni kwetu kwa sababu soko ndani mwao linajitosheleza.
 
Hizo ndizo zilizo kwenye soko, zinajulikana na wengi ila US wana kampuni inaitwa Harley davidson ni balaa hatuzioni kwetu kwa sababu soko ndani mwao linajitosheleza.
Harley Davidson [emoji91]
Bmw
Ducat
Yamaha
Honda
 
Back
Top Bottom