Wadau wa Uongezaji Thamani Madini Waitikia Wito wa Serikali Kuwekeza Kwenye Viwanda vya Uchenjuaji Madini Nchini

Wadau wa Uongezaji Thamani Madini Waitikia Wito wa Serikali Kuwekeza Kwenye Viwanda vya Uchenjuaji Madini Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WADAU WA UONGEZAJI THAMANI MADINI WAITIKIA WITO WA SERIKALI KUWEKEZA KWENYE VIWANDA VYA UCHENJUAJI MADINI NCHINI

-Waziri Mavunde akutana na Kampuni ya MAST na AKMENITE

-_Viwanda vya Uchenjuaji madini kujengwa Ruvuma,Dodoma,Katavi na Lindi _

-Ujenzi wa viwanda kuanza mapema mwaka huu

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amekutana na kufanya mazungumzo wadau wa Sekta ya Madini kutoka Kampuni ya Mineral Access System Limited(MAST) ikiwakilishwa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw Georgefrey Kente pamoja na Mwekezaji toka Lithuania, Bw. Arunas Sermuksnis; Mkurugenzi wa kampuni ya Akmenite Limited ambao wote wameonesha nia kuanzisha ujenzi wa viwanda vya uchenjuaji wa madini ya metali kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza thamani madini nchini.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa Kampuni ya MAST Ndg.Georgefrey Kente ameonesha utayari wa kampuni yake kujenga viwanda vitatu vya uchenjuaji wa madini ya metali katika mikoa ya Ruvuma,Dodoma na Lindi ambapo ujenzi wake unatarajiwa kuanza mapema mwaka huu ambapo jumla ya zaidi Dola za kimarekani 15m USD zitatumika kukamilisha ujenzi huo.

Naye Bw. Arunas Sermuksnis; Mkurugenzi wa kampuni ya Akmenite Limited naye amehakikishia serikali kwamba wataleta nchini teknolojia ya kisasa ya uchenjuaji wa metali ili shughuli za uongezaji madini kufanyika ndani ya nchi na hatua za awali za uanzishwaji wa kiwanda hicho zimeanza tayari.

Naye Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amezipongeza Kampuni hizo kwa uamuzi huo wa kuwekeza viwanda vya uchenjuaji madini ndani ya nchi na kuhimiza ukamilishaji wake uwe ndani ya muda mfupi ili wachimbaji wa Tanzania wanufaike na fursa hiyo kwakuwa kwa hivi sasa moja ya changamoto kubwa inayowakabili Wachimbaji wa madini ya metali ni kukosekana kwa teknolojia ya uchenjuaji ili kutosafirisha madini ghafi nje ya nchi.

Waziri Mavunde pia amewahakikishia wawekezaji hao kwamba serikali kupitia Wizara ya Madini itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kwamba uwekezaji huu unafanyika kwa manufaa ya maendeleo ya sekta ya madini Tanzania.

Aidha wadau hao wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji na kuwajali wachimbaji wadogo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.11.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.11.jpeg
    92.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.12.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.12.jpeg
    94.8 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.12(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.12(1).jpeg
    70.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.12(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.12(2).jpeg
    113.3 KB · Views: 0
  • WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.13.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.13.jpeg
    106.9 KB · Views: 0
  • WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.13(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.13(1).jpeg
    75.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.14(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.14(1).jpeg
    53.9 KB · Views: 0
  • WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.14(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.14(2).jpeg
    87.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.15.jpeg
    WhatsApp Image 2024-04-23 at 17.06.15.jpeg
    94.8 KB · Views: 0
Back
Top Bottom