Wadau wanahoji kama mchakato wa 'transformation' wa Simba umekamilika, vipi kuhusu Yanga?

Wadau wanahoji kama mchakato wa 'transformation' wa Simba umekamilika, vipi kuhusu Yanga?

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Wakuu,

Kumekuwa na hoja ya wadau mbalimbali wa michezo, wanachana wa Simba na wasio Simba. Watu wanataka kujua nini kinakwamisha mchakato wa transformation kukamilika pamoja na uhalali wa Mo Dewji kuwekeza hisa 49% peke yake.

Yanga wapinzani wao wa jadi nao wapo kwenye mchakato wa kubadilisha uendeshaji wa Klabu yao kama ilivyo Simba.

Maswali nayojiuliza ni:

Je, Yanga wamekamilisha mchakato wao?

Kama bado kwanini waandishi hawahoji kuhusu Hilo?

Kama si halali kwa Mo Dewji kumiliki hisa 49% Simba je GSM atamiliki na nani kwa Yanga?

Wanaojua suala hili naombeni ufafanuzi.

Nawasilisha
 
Salaam Wakuu,

Kumekuwa na hoja ya wadau mbalimbali wa michezo, wanachana wa Simba na wasio Simba. Watu wanataka kujua nini kinakwamisha mchakato wa transformation kukamilika pamoja na uhalali wa Mo Dewji kuwekeza hisa 49% peke yake...
Tumalize kwanza upande wa Simba kwa sababu karibu wagawane mbao!

Sijui shabiki lao namba wani GENTAMYCINE lina hali gani, si ajabu lipo ICU likiwa njiani kwenda mochuari! 😭😭😭
 
Kinacho leta utata Simba ni kwamba ina ishi kwenye mfumo wa transformation wakati bado haija kamilika hapo ndio chanzo cha tatzo huko Yanga sijasikia kama GSM ana miliki hisa huku kwetu Mo leo muwekezaji kesho mmiliki mara kaweka 20B mara hajaweka ni vurugu
 
Salaam Wakuu,

Kumekuwa na hoja ya wadau mbalimbali wa michezo, wanachana wa Simba na wasio Simba. Watu wanataka kujua nini kinakwamisha mchakato wa transformation kukamilika pamoja na uhalali wa Mo Dewji kuwekeza hisa 49% peke yake...
Yanga mbona hata kwenye mkutano mkuu juzi hapa imesemwa. Mchakato wa mabadiliko unaendelea. Kilichopo sasa ipo kamati ya mabadiliko ambayo inafanya tathmini ya thamani ya Klabu.

Walitangaza tenda na wamepata kampuni tatu. Wakipata thamani ya Klabu sasa ndiyo wanatangaza kutafuta mwekezaji. Simba sijui thamani ya timu yao waliijuaje.
 
Kumekuwa na hoja ya wadau mbalimbali wa michezo, wanachana wa Simba na wasio Simba. Watu wanataka kujua nini kinakwamisha mchakato wa transformation kukamilika pamoja na uhalali wa Mo Dewji kuwekeza hisa 49% peke yake.
Mchakato wa transformation simba ulikwamba kwasababu kwenye katiba kulikua na vipengere ambavyo mamlaka za usajiri ziliamuru vibadilishwe moja ya kipengere ni kwamba katika zile hisa 49% upande wa mwekezaji kunatakiwa kuwa na wqwekezaji angalao watatu kitu ambacho ni tofauti na katika ambayo simba aliipeleka ambapo hisa 49% alikuwepo Mo peke ake
Je, Yanga wamekamilisha mchakato wao?

Kama bado kwanini waandishi hawahoji kuhusu Hilo?
Mchakato wa mabadiliko yanga umeshakamilika hatua ya kwanza ilikua kupata viongozi ambapo injinia alishinda kuwa rais wa timu kwa sasa mchakato upo kwenye hatua ya kufanya calculation ya thamani ya timu ili hisa ziweze kuuzwa kwa wawekezaji watakaojitokeza
Kama si halali kwa Mo Dewji kumiliki hisa 49% Simba je GSM atamiliki na nani kwa Yanga?
Hakuna popote ambapo GSM imepewa ulazima au upendeleo katika kumiliki yanga, kwa sasa GSM bado ni mfadhiri na business partner tu pale yanga(ana tenda ya kutengeneza na kusambaza vifaa vya michezo kwa logo ya yanga). Thamani ya timu ikishajulikana na wawekezaji kupewa ruhusa ya kununua hisa basi GSM pamoja na wawekezaji wengine wote watakaribishwa.
 
Yanga mbona hata kwenye mkutano mkuu juzi hapa imesemwa. Mchakato wa mabadiliko unaendelea. Kilichopo sasa ipo kamati ya mabadiliko ambayo inafanya tathmini ya thamani ya Klabu.

Walitangaza tenda na wamepata kampuni tatu. Wakipata thamani ya Klabu sasa ndiyo wanatangaza kutafuta mwekezaji. Simba sijui thamani ya timu yao waliijuaje.
Simba thamani ya klabu yao waliambiwa na Kanjibhai mwenyewe kwamba ni bilioni 20, akuna chombo chochote Cha maana kilichofanya tathmini ya kujua thamani ya Simba, yaani aliwashika masikio na wenyewe wakajaa kwenye mfumo wake, Leo unamsikia anasema ameshainunua Simba sijui aliuziwa na try again ama nani!
 
Umeanza kwa kusema wadau wanahoji, ila ukaishia kutaja maswali unayojiuliza binafsi..... hebu malizaneni huko huko bila kumtaja jirani.
 
Back
Top Bottom