Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) ambayo huadhimishwa kila 27,Februari, mjadala kuhusu hali inayokabili sekta ya AZAKI imekuwa gumzo hasa kutokana uamuzi wa hivi karibuni wa Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kusitisha baadhi ya misaada ambayo imekuwa ikitolewa Taifa hilo .
Wadau mbalimbali wakizungumza katika Mkutano ambao uliandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wa kimkakati ambao umewaleta pamoja baadhi ya Viongozi AZAKI kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ukiwa na lengo la kujadili changamoto zinazokabili sekta hiyo nchini wamebainisha changamoto ya upatikanaji wa rasilimali fedha inayowezesha utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
View: https://youtu.be/ZrwcFJaG3pw?si=VdPUIEwJSeC6p30a
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Februari 28, 2025, Mratibu Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema changamoto kubwa inayozikumba AZAKI nyingi ni ukosefu wa rasilimali zinazoweza kuendesha taasisi hizo bila kutegemea misaada kutoka nje.
Ambapo amesema kuwa mangura hayo yanazifanya taasisi hizo kushindwa kutoa huduma kwa ukamilifu kwenye jamii pale wafadhili wa nje wanapokata misaada, akitolea mfano kama ilivyotokea kwa serikali ya Marekani ambayo imesitisha misaada kwa Nchi za nje ikiwemo Tanzania.
Olengurumwa amesema ili kuhakikisha AZAKI zinasimama imara hata wafadhili wa nje wanaposiitisha ufadhili wao ni lazima uwekwe mikakati ya kutafuta rasilimali za ndani(DRMC) ambazo zitasaidia katika kushughulikia matatizo mbalimbali ya kijamii.
Aidha Dkt John Kalaghe ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Uhamasishaji wa Rasilimali za Ndani (Domestic Resource Mobilization Commitee-DRMC), amesema THRDC ilizindua mkakati huo mwaka 2024 ingawa maendeleo yake yanaenda taratibu.
Amesema kuwa matarajio yaliyopo kutokana na changamoto za ufadhili wa nje zinazoendelea kutokea siku za hivi karibuni, ni kwamba zinatoa nafasi ya kuongeza kasi na juhudi kuhakikisha utekelezaji wake pamoja na Mapendekezo ya OECD/DAC.
Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya fedha zote zinazotolewa na nchi 32 wanachama wa DAC (Mapendekezo ya DAC ni miongozo iliyotolewa na Kamati ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi na Maendeleo (Development Assistance Committee – DAC) ya OECD, ambayo inalenga kuboresha ufanisi wa misaada ya maendeleo kwa nchi zinazoendelea) ni 7% pekee zinazofikia AZAKI za ndanu huku 93% zikienda kwa wafadhili wa nchi hizo na NGOs za Kimataifa.
Aidha, takwimu za hivi Karibuni zinaonyesha kuwa ni 25% pekee ya ufadhili wa serikali ya Marekani kupitia USAID unaofikia AZAKI za ndani, huku 75% ikienda kwa INGOs na taasisi za ndani zinazofadhiliwa kutoka nje.
Hata katika uchangiaji hoja baadhi ya wachangiaji wameunga mkono kuwepo kwa mkakati wa kutafuta rasilimali za ndani ili kuwezesha wadau hao kuweza kutekeleza majukumu yao.
Ikumbukwe hivi karibuni THRDC ilitoa taarifa ya utafiti wa awali baada ya Marekani kutangaza kusitisha misaada, ambapo katika taarifa ya mtandao huo mwamvuli wenye Wanachama takribani 300 Tanzania Bara na Zanzibar walibaini athari katika sekta ya AZAKI hali ambayo walidai kuwa inaziweka AZAKI nyingi katika ugumu wa kuendelea kutekeleza majukumu yake kama ilivyozoeleka.