Wadau zaidi ya 1000 kukutana Zanzibar kujadili namna matibabu ya matatizo ya moyo yanavyoweza kupatikana kwa urahisi Afrika

Wadau zaidi ya 1000 kukutana Zanzibar kujadili namna matibabu ya matatizo ya moyo yanavyoweza kupatikana kwa urahisi Afrika

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Wadau zaidi ya 1000 kutokea mataifa takribani 40 hususani ya Afrika wanatarajiwa kukutanishwa Zanzibar na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), April 2025 katika mkutano wa tatu ambao utalenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kufanikisha urahisi wa matibabu yanayohusisha matatizo ya moyo kupungua.

IMG_5670.jpeg

Akizungumzia mkutano huo August 13, 2024 mbele ya wadau mbalimbali, Mwenyekiti wa maandalizi ya mkutano huo, Dkt. Delilah Kimambo amesema kuwa lengo kubwa la mkutano huo ni pamoja na kukusanya wataalamu katika sekta ya matibabu ya moyo kujadili mada zitakazohusiana na kinga lishe na matibabu ya moyo, na kuibua mikakati ambayo itawezesha matibabu ya matatizo ya moyo yaweze kupatikana kwa urahisi.

"Kupitia mkutano wetu wa Kimataifa wa magonjwa ya moyo tunaenda kujadili kuona jinsi gani tunaweza kusaidia Afrika kwa njia rahisi kabisa ili matibabu ya moyo yaweze kupatikana kwa urahisi"amesema Dkt.Delilah

Ameongeza pamoja hayo lakini kupitia mkutano huo kwa mara ya kwanza JKCI itaenda kushirikiana na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kuwafundisha Watu ambao sio wataalamu wa afya jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa anayehitaji huduma hiyo na kuwaleta watu pamoja.

Pia akizungumzia mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika katika hotel ya Sea Cliff & Spa Visiwani Zanzibar, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge amesema kupitia mkutano huo wataalamu wa afya watafundishwa matumizi ya teknolojia mpya katika kutibu magonjwa ya moyo kwa kutumia njia za kisasa akiwemo akili mnemba.

Ameongeza kuwa mkutano huo utaenda sambamba na kutoa mafunzo ya kutoa huduma za dharura kwa wangoza watalii na wahudumu wa kwenye hoteli kutoka Zanzibar ambapo mkutano huo utafanyika, amesema kuwa suala hilo ni hatua kubwa kwa sababu wanaoenda kunufaika na mafunzo hayo ni Watu wa aina zote sio kama ilivyozoeleka mafunzo hayo kutolewa haswa kwa wataalamu wa kada ya afya pekee.

Aidha Kaimu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Aziwa Issa Makame amesema kuwa mkutano huo utaenda kuchochea ongezeko la Watalii Zanzibar, lakini pia amesema kuwa utaleta tija ya huduma kwa wanaongoza watalii ambao watanufaika mafunzo ambayo watakuwa wakiyatumia kusaidia watalii upatwa na changamoto za kiafya.

Hata hivyo ametoa wito kwa wadau kutoa ushirikiano katika mkakati huo ili kuwezesha wahudumu hao kupata mafunzo pamoja na kushiriki ipasavyo katika maandalizi ya mkutano huo.
 
Back
Top Bottom