Arnold Kalikawe
Senior Member
- Sep 28, 2016
- 152
- 374
Miaka ya 2000 kulikuwa na wanamuziki wanne wenye majina makubwa ambao hao waliamua kuwaita kwa jina la Big Four yani Jay Z, Nelly, DMX na Eminem. Huyu jamaa unayemuona kwenye picha aliibuka tu na kuanza kupiga kelele mitaani na Mixtape yake fulani hivi.
Hakuna yeyote kwenye hii Big Four aliyetamani kumgusa kwa sababu ya kukubalika huko mitaani. Halafu jambo baya likatokea, akapigwa risasi tisa mwilini mwake. Kila mmoja aliamini amekufa, amepotezwa milele.
Miezi mingi ikapita, eeeh! Jamaa huyu hapa amerudi na Mixtape nyingine. Ila katika kipindi hiki, miongoni mwa watu walionunua hiyo Mixtape alikuwa Paul Rosenberg (Huyu alikuwa ni meneja wa Eminem, aliinunua kwa ajili ya kwenda kumsikilizisha mshikaji amsikie kijana).
Akampa Eminem.
Katika moja ya interview Eminem alisema:
“Nilichokuwa najua ni kwamba 50 alipigwa risasi, na kila mmoja mpaka tasnia ya muziki ikajua jamaa alikufa hapohapo. Halafu baadaye Paul akanipa mixtape yake mpya, nakumbuka nilimuuliza, 50 Cent bado anarap?, akaniambia, nenda kaisikilize tu. Na nikafanya hivyo. Kitu cha kwanza nilichomwambia Paul, Huyu dogo ni hatari.”
Eminem akapendezwa nayo, akaona haiwezekani, ikabidi amtafute 50 na kumpa beat kwa ajili ya kufloo nayo, alitaka kuona ni kwa namna gani alikuwa na uwezo huo. 50 akapiga verses mbili matata na kumpa Eminem, naye akaongezea verse moja, hiyo ngoma ikaitwa Patiently Waiting.
Eminem akawasiliana na Dr. Dre na kumwambia kuhusu 50 Cent, akamwamini na hivyo kumsaini kwenye lebo yake ya Shady Record na Dre akaprodyuzi nusu ya albamu huku nusu ikiwa produced na Eminem chini ya Aftermath.
Baada ya kila kitu, baadaye ikaandaliwa In Da Club. Ngoma ikatoka, ikawa BOOOM. Yaani ninaposema BOOOOM ni BOOOM kweli.
Ikasikika dunia nzima, ikampa pesa nyingi, umaarufu wa kumwaga mpaka leo hii.
Kama 50 hajakuinspire kwenye safari yake ya mafanikio, nadhani hakuna chochote kile kitakachokuinspire.o