Wadukuzi wa kimtandao walivyozua taharuki kwa mashabiki wa muziki duniani

Wadukuzi wa kimtandao walivyozua taharuki kwa mashabiki wa muziki duniani

Robidinyo

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
4,043
Reaction score
8,686
Mwaka 2017 Allikiba na Baraka de prince ni miongoni ya wasanii waliyolalamikia kuhujumiwa video zao Youtube kwa kusababisha views ku stuck na kuto ongezeka na kupelekea management ya.Alikiba ikiongozwa na Seven Mosha na Haidan Charle kuwasiliana na makao makuu ya youtube kuhoji nini tataizo

na kufikia mashabiki wa Kiba kulaani WCB na kuwahusisha kuhujumu video ya Kiba

Huku Baraka de prince akigombana na MX Carter ambae alikuwa ni admin waYoutube account yake kupitia kampuni ya Ngomma Vas inayo jishughulisha na ku manage account nyingi za wasanii bongo za Youtube

Hadi kufikia Baraka kuvunja mkataba na kampuni hiyo.

Ila wengi wanafikiri swala hili kutokea ni jambo la ajabu, ki uhalisia hili Swala mtambuka kwani si mara ya kwanza kutokea....

Tukirudi miaka kadhaa video pendwa na iliyovunja record ya kutazamwa mara nyingi zaidi(6.6 billion views) kwenye paltform ya Youtube ‘Despacito’ ya Luis Fonsi and Daddy Yankee iliwai kudukuliwa(hacked)

Story iko hivi...

Asubuhi mapema ya tarehe 10 April 2018,Jumanne mashabiki wa muziki kote duniani walishangazwa na tukio la ghafla amabapo walikuta video ya despacito ikiwa na thumbnail(picha inayowakilisha video youtube) ikiwa ibadilishwa na kuwekwa picha ya series maarufu ya kiispania ‘Money heist’ na kubadilishwa caption kutoka maneno ya awali na kuwekwa majina ya wadukuzi wawili wa kiarabu yaani Prosox and Kuroi’sh

wakijitambulisha kama wadukuzi na kuongezea neno “free palestine” wakiwa na maana palestine iachwe huru na kutambulika kama taifa linalo Jitegemea,
Huku ikifatiwa na kudukua account nyengine za video vevo zikiwemo video za Shakira’s “Chantaje,” Selena Gomez, Drake na Taylor Swift ziliathiriwa na Wadukuzi hao pia hawakuishia hapo

pia walidukua official website.tukio hilo ilibidi Vevo wazizuie account zote zilizo athirika kwa muda huku mwakilishi kutoka Vevo,Remezcla alikaliliwa akisema kuwa “ Vevo can confirm that a number of videos in its catalogue were subject to a security breach today, which has now been contained”

huku msemaji wa Vevo .Kutoka Youtube anabaye ni mshirika wa Vevo Aliongezea na kusema “After seeing unusual upload activity on a handful of VEVO channels, we worked quickly with our partner to disable access while they investigate the issue.”

Wadukuzi hao pia wiki kabla ya tukio hilo walifanikiwa Kudukua tovuti maarufu za habari zenye za twitter za nowthisnews na bbcarabicalerts,na baada ya muda accounts zote za wasanii zilizo dukuliwa zilirudi kama awali, ila jambo la kushangaza zaidi ni kuwa
Account za twitter zinazo aminikia ni zao hao wadukuzi wa ki Iran

walisema kuwa, na nukuu “Vevo kwa heshima zote tulichokifanya kilikuwa kama utani,muwe makini, tulifanya kama mchezo tuu kama tungekuwa serious tungeliweza kufuta video zote za wasanii hao ila hatukufanya hivyo” pia kwenye mwendelezo wa tweet walisema “Youtube Its just for fun i just use script "youtube-change-title-video" and i write "hacked" don t judge me i love youtube [emoji3531]”

Mpaka leo wadukuzi hao hawajawai kukamatwa bali wameacha maswali kwenye vichwa vya wataalamu wengi wa tehama duniani na13.Hawa waliwezaje kujipenyeza na Kuingia kwenye account hizo kirahisi namna hiyo?
-MWISHO

@Chapo255
#SanukanaChapo

Hapa Jf imeletwa kwenu na Robidinyo (Spartcus The Mnyama Mkali)
IMG_20200410_140316.jpg
View attachment 1415096View attachment 1415094View attachment 1415095
 
1586521340303.png

Hakuna cha views ku stuck wala kuto ongezeka wala kushuka.

Yaani video ya dodo ya Ali kiba ilapataje pataje views milioni 1 ndani ya masaa manane, Hiki kitu hata msanii mkubwa wa hapa afrika mashariki hajawahi kupata, sanasana anapata views milioni ndani ya siku lakini sio kwa masaa 8.

Kuna kitu kinaitwa invalid views yyani views hewa, unakuta mtu ana simu elfu tano huko china anaombwa aongezee views ila youtube wakawa wajanja wana system ya kuzijua hizi views feki na hata ukipata views milioni 10 kwa saa usishangae zikichujwa upate views elf 2
 
View attachment 1415182

Acha kudanganya we Guruguja Alikiba katoa wimbo Juzi tarehe 8 mida ya saa 5 asubui Views 1m Zimetimia Jana Jioni

Ebu piga hesabu vizuri na elimu yako ya shule za kata hayo ni masaa 8?
 
[emoji23][emoji23][emoji23]kwahiyo huyo mtu analipwa shilingi ngapi???ambayo inapatikana kwa ingizo baada ya kuangalia hizo video youtube!!!

na hizo fake cricks zinashtukiwaje ikiwa kila simu ina email yake kama ambavyo inakuwa kwa watazamaji wa kawaida????,na vipi unafikiri ni rahisi kuwa na simu walau mia tu,kwa ajiri ya kuongeza view 100???si ni ujinga huu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kudanganya we Guruguja Alikiba katoa wimbo Juzi tarehe 8 mida ya saa 5 asubui Views 1m Zimetimia Jana Jioni

Ebu piga hesabu vizuri na elimu yako ya shule za kata hayo ni masaa 8?
Views feki ziliingia milioni baada ya masaa 8 za ukweli ziliingia siku inayofata
 
Acha kudanganya we Guruguja Alikiba katoa wimbo Juzi tarehe 8 mida ya saa 5 asubui Views 1m Zimetimia Jana Jioni

Ebu piga hesabu vizuri na elimu yako ya shule za kata hayo ni masaa 8?
Ila nimekusifu umetoa credit kwa muandika makala asilimia kubwa ya members wa jamiiforum wanaleta mada zilizondikwa makala na mtu fulani bila kutoa credit wanajifanya wameandika wao.
 
Back
Top Bottom