Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kuna Waethiopia kadhaa (inadaiwa wapata 100) ambao walikamatwa huko Arusha mapema mwaka huu wakiwa njiani kuelekea Afrika ya Kusini kutafuta maisha kwa kuingia nchini kinyume cha sheria na sasa wameamua kugoma kula na hali zao ni dhaifu sana. Umri kati ya vijana hao ni kati ya miaka 16 na 25.
Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Masha na serikali ya TAnzania inaonekana haijui ifanye nao nini kwani hadi hivi sasa serikali ya Ethiopia haijaonesha utayari wa kuwapokea watuhumiwa hao wa uhamiaji haramu. Upande mwingine serikali inaonekana kudai kuwa si jukumu lao kuwarudisha hawa watu nchini mwao na ni kutokana na hilo watuhumiwa hao wameamua kugoma kula.
Kutokana na udhaifu wao baadhi yao wanatarajiwa kukimbizwa hospitali ya Mt. Meru wakati wowote kwa ajili ya kunusuru maisha yao. Waziri Masha anatarajiwa kuelekea Arusha wakati wowote ndani ya masaa 72 yajayo kujaribu kutafuta suluhisho la matatizo ya wahamiaji hao.
Fluid: