Wafahamu Celebrities waliotoka familia bora

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Hakuna mtu asiyejua maana ya watoto wa kishua basi kama yupo basi maana halisi ya neno hili ni wale watoto waliozaliwa kwenye familia zinazojiweza au unaweza kuita familia Bora. Mara nyingi wasanii wengi huwa wanatokea maisha duni na kupigana na maisha hadi kufikia walipo sasa. Kipindi Diamond akiacha shule kwa kukosa pesa ya kumsomesha nana elimu yake kuishia A'level , Hawa wengine walikua wapo shule wakisoma na kuishi vizuri. Hawa ndo baadhi ya watoto wakishua ambao kwasasa ni celebrities…

Vanessa Mdee
Vanessa Hau Mdee au unaweza kumuita Vee au Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa mdee alikuzwa na baba yake Sammy Mdee (kwasasa ni marehemu )ambaye alikua ni mtu mzito kwenye nchi hii na mama yake sophia. Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris , Nairobi na Arusha.

Nisher
Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. Nisher
amekulia katika maisha mazuri na hadi ni wakishua bado. Baba yake aliweza kumsaidia Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni 15 ili mtoto wake aendeleze kipaji alichonacho.

Jokate Mwengelo
Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini. Kumbuka Jokate alizaliwa washington DC nchini Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza high school katika shule ya Loyola ndipo alipogombania Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2.

Lucci
Jina lake halisi anaitwa Luciano Tsere au unaweza kumuita Lucci ambaye ni producer maarufu nchini. lucci amezaliwa tarehe 30 September mwaka 1985 Lusaka Zambia, akiwa ni mzaliwa wa nne, wa mwisho kuzaliwa na akiwa mtoto wa kiume pekee kwenye familia yao. Lucci naye kama jokate amekulia Obey kwenye familia bora ambapo kwasasa mzee wake ni balozi wa Tanzania.

Wema Sepetu
Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi Isaack Sepetu Ibrahimu (marehemu).Wema Sepetu alizaliwa mnamo mwaka 1988 katika hospitali ya ST. Andrew's jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa mwisho kuzaliwa huku akisoma elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda
Nchini Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha Limkokwing University.
 
Duh! Kumbe ka'wema ka mwaka 88 alafu umemsahau king crazy gk nae si mtoto wa kishua? Au tulikalilishwa?
 
Crazy GK nae mtoto wa upanga - akina FA walikuwa wanapewa hifadhi nao wakajiita wakishua Baba ake alikuwa kigogo na mama ake ni mbunge wa viti maalum Chadema. AY nae alikuwa wakishua babake alikuwa kigogo pia serikalini
 
we katalina hii ni celebrities forum unataka tujadili nini.
majukwaa yako mengi Jf unaweza kwenda huko kwa rich minds muache binamu

Ivi diva binamu na yeye sio mtoto wa kishua kweli yule??
 
Crazy GK nae mtoto wa upanga - akina FA walikuwa wanapewa hifadhi nao wakajiita wakishua Baba ake alikuwa kigogo na mama ake ni mbunge wa viti maalum Chadema. AY nae alikuwa wakishua babake alikuwa kigogo pia serikalini

Gk sio wa kishua muda mwingi anaishi na mama yake ambae maisha yake yote alikua mwalimu wa sekondari mpaka alipopewa ubunge na chadema. Msikariri kuish upanga ndio mambo safi.hao kina ay, buff g, snare na fa wote ndio walewale sema wao wazazo wao waliuza sijui walipangisha nyumba zao hivyo wakawa sio wazawa tena wa upanga
 
Za mani washua walikaa obey, upanga , Masai. Badala ya serialized kuuza nyumba sake siku hivi familia za Keisha zina ishi wapi..
 
Kayaman mamake GK alifundisha Tambaza sekondari A level somo la GS miaka ya 2000's
 
Ila ana ung'eng'e mtamu madam anasubir , si nasikia mtoto wa mikochen yule aka mtoto wa malinz

Awe wakishua atambe.. huko mikocheni kahamia juzijuzi kakulia moro yule tena kalelewa na mama huyo babake mzazi kamjulia uzeeni tena baada ya kwenda mjengoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…