Wafahamu kuwa mkojo wa wanyama una mbolea kuliko kinyesi chake?

Wafahamu kuwa mkojo wa wanyama una mbolea kuliko kinyesi chake?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kinyesi ni makapi ya chakula baada ya umeng'enyaji kwenye mfumo wa chakula. Mkojo wenyewe ni mkusanyiko wa taka mwili karibu zote za mwilini. Taka hizo zinatoka mwilini mwote, zinaingia kwenye damu, kwenye figo na kisha kama mkojo. Hivyo mkojo unakuwa na makorokoro mengi sana ukilinganisha na kinyesi. Moja ya makorokoro hayo kwa wingi ni Nitrogen.

Wanyama kama ng'ombe wanaokula nyasi tu mbolea yao ni daifu sana. Ni makapi yenye virutubisho vichahche kwa ajili ya mmea. Kuna wanyama kama ndege au popo ambao mfumo wa mkojo na kinyesi umechanganyikana. Wanyama hawa mbolea yao ina madini mengi sana sababu ina mchanganyiko wa virutubisho kutoka kwenye kinyesi na mkojo.

Ukitaka kinyesi cha wanyama kama ng'ombe kiwe na mbolea basi kichanganye na mkojo wake. Kwenye zizi chini tandika nyasi. Ng'ombe wanapojisaidia mkojo na kinyesi vitachanganyikana kwenye nyasi. Nyasi hizo zitakuwa mbolea nzuri kama ile ya ndege.
 
Back
Top Bottom