Wafahamu viumbe sita wanaolala jicho wazi

Wafahamu viumbe sita wanaolala jicho wazi

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Kulala huku macho yakiwa wazi huwasaidia wanyama kuwa macho dhidi ya hatari zinazoweza kutokea na kuwawezesha kujibu mapigo inapohitajika.

Ni maisha ya kuvutia ambayo huwaruhusu kupata hitaji la kupumzika na hitaji la usalama katika eneo lao.

Hawa ni baadhi ya wanyama ambao hulala jicho moja likiwa wazi.

MAMBA.jpeg


MAMBA
Watafiti wamethibitisha mamba huacha wazi jicho moja na kulala kwa jicho lingine.
SUNGURA.jpeg


SUNGURA
Hulala kwa jicho moja, lakini si mara zote hususani wakiwa porini ili kujikinga na Wanyama wanaowawinda wakiwemo binadamu.

NYANGUMI.jpeg


NYANGUMI
Kulala na jicho moja wazi huruhusu kuja juu inapohitajika ili kupata hewa. Wakati jicho moja limelala, lingine linatazama mazingira.

POPO.jpeg
POPO
Hulala jicho likiwa wazi lakini jambo la ajabu ni kwamba, hulala mchana kichwa chake kinaning’inia na hupaa usiku.

POMBOO.jpeg
POMBOO
Ni mmoja wa mamalia wanaoishi baharini, anajua jinsi ya kufunga nusu ya ubongo wake. Maana yake analala jicho moja tu, huku lingine likiwa wazi.

MWARI.jpeg
MWARI
Hulala kwa jicho moja tu, huku lingine likitazama wawindaji au maadui. Lengo kuu ni kupumzika na kufahamu maadui.
 

Attachments

  • POMBOO.jpeg
    POMBOO.jpeg
    107.5 KB · Views: 7
Back
Top Bottom