Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 97
- 72
Katika hii dunia, tunao watu wajinga sana wa aina mbili:
Nilisikika katika ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikitema cheche, nikiuonyesha ulimwengu jinsi ninavyokerwa na mambo ya kijinga jinga. Nikaanza:
Nakumbuka tarehe 28/02/2024, Prophet IPM, nabii Mkristo aliyetokea kwenye imani ya Kiislamu na mwenye kanisa lake huko Mbezi Beach Mbuyuni, alisema:
"Naomba unisikilize vizuri na unielewe. Hakuna mwanadamu mwenye akili timamu asilimia 100. Na hakuna mwanadamu chizi asilimia 100. Nisikilize tu kidogo hata kwa hizi akili zangu ndogo. Unisikilize tu."
Mwisho wa kunukuu.
CCM inatambua haya, na ndiyo maana ukisoma vitabu vyao kuna kukosoana. Tusome:
"Integrity ni jambo muhimu sana. Ni vizuri hizi kanuni tuzisome. Sasa mnatakiwa kuziishi, sio kuzisoma tu, bali pia kuziishi na kuzitekeleza."
Mwisho wa kunukuu.
Tusome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, toleo la 2005, ukurasa wa 13, aya ya kwanza, na ibara ya 12(1)(2), ibara ya 13(1)(4)(5).
Nchi yetu itapiga hatua endapo tutajipa ujasiri wa kukemea adui ujinga, ambaye ndiye adui namba moja aletaye umasikini na maradhi.
Kila kukicha, ujinga unatufanya tuzidi kuwa wanyonge, na wanaopaswa kutupa elimu wamegundua njia pekee ya kutudhulumu ni kutumia makundi ya watu wajinga, kuyawalisha ubwabwa na kisha wajinga hao kujizima data na kushangilia lolote na chochote.
Huku majina mengi yakiwa na ujinga wa kutojua ilani, katiba, kanuni, miongozo, na taratibu za kimfumo, yanakubali kushiriki vitendo vya kipumbavu kwa ahadi ya ubwabwa. Badala ya kutafuta elimu na maarifa, yanashirikiana kumkejeli mtu anayejitahidi kuyasaidia kutoka kwenye dimbwi la ujinga.
Tuisome Katiba ya CCM ya mwaka 1977, toleo la 2022:
Akiwa SUA, Morogoro, tarehe 07/05/2018, alisema:
"Tulikuwa tumejenga element ya kudanganya kila kitu. Sasa element hii ni lazima tuibadilishe katika maisha yetu. Sisi Watanzania tujifunze kusema ukweli."
Adui ujinga humwingia na kumuishi mtu bila kujali cheo au kipato. Ujinga upo kila sekta.
Akiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya uzinduzi wa Chuo cha Ufundi Stadi huko Kagera, tarehe 13/10/2022, alisema:
"Mwasisi wetu wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere, katika wakati wake alipigania uhuru wa nchi yetu. Na baada ya kupata uhuru, alisema mambo matatu makubwa: la kwanza ni njaa, lakini pia ujinga na maradhi. Mwalimu alisema hawa ni maadui watatu wakubwa wa Taifa letu, na katika wakati wake aliyafanyia kazi kwa kiasi kikubwa."
"Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa analinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alikuwa anailinda katiba."
================================================
(Baadhi ya Viongozi) Wasitumie Mwalimu Kama Hirizi
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alichokuwa akisema, pia alikuwa anatenda. Hawa (baadhi ya viongozi) wanasema kimoja lakini wanatenda kinyume kabisa na jinsi ambavyo Mwalimu angefanya.
Ndani ya Nchi:Mheshimiwa Rais akishasema, sisi ni utekelezaji. Hata hivyo, tunashuhudia mambo ya kijinga. Watu wanapinda mifumo, wanapeana vyeo kiholela. Tunayaona, lakini kwa ujinga tunapewa vitisho, tunawachekea viongozi wasio stahili. Matokeo yake, tunaona watu hawasomi mapato na matumizi huku wakilindwa kwa gharama zote. Sisi wasema kweli, tunatengwa na kuwindwa.
Dkt. Damas Daniel Ndumbaro - Waziri wa Katiba na SheriaNakumbuka tarehe 12/10/2022 alisema:
Kuwajibika Kama Wazalendo:Tunawezaje kujiita wazalendo ikiwa tuliapa kutokupendelea, lakini sasa tunapendelea watu mchana kweupe kana kwamba hatukuapa wala kushika vitabu vya Mwenyezi Mungu? Tumeshiriki kwa kiasi gani kuondoa mambo haya ya kijinga yanayokiuka viapo na kuviza haki za mafukara? Twawezaje kusema tuna akili ikiwa tunakiuka viapo vyetu na kisha kukimbilia kwa watumishi wa Mungu tukitaka kuombewa?
Mwalimu Nyerere Alisisitiza:Mwalimu alisema:
- Wajinga wenye kaujanja fulani, wenye uwezo wa kupewa elimu na kuacha ujinga.
- Wajinga wenye upumbavu wa kuwatotosha, uliowasahaulisha Mwenyezi Mungu na kuwafanya kujihisi kuwa na kauungu ndani yao.
Nilisikika katika ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikitema cheche, nikiuonyesha ulimwengu jinsi ninavyokerwa na mambo ya kijinga jinga. Nikaanza:
Nakumbuka tarehe 28/02/2024, Prophet IPM, nabii Mkristo aliyetokea kwenye imani ya Kiislamu na mwenye kanisa lake huko Mbezi Beach Mbuyuni, alisema:
"Naomba unisikilize vizuri na unielewe. Hakuna mwanadamu mwenye akili timamu asilimia 100. Na hakuna mwanadamu chizi asilimia 100. Nisikilize tu kidogo hata kwa hizi akili zangu ndogo. Unisikilize tu."
Mwisho wa kunukuu.
CCM inatambua haya, na ndiyo maana ukisoma vitabu vyao kuna kukosoana. Tusome:
- Kitabu cha Kanuni za Uchaguzi wa CCM, toleo la Desemba 2022, ukurasa wa 2-4, ibara ya 5(1).
- Katiba ya CCM, ibara ya 15(7).
- Mwongozo wa CCM 1981, ukurasa wa 51-52, ibara ya 65, na ukurasa wa 45-46, ibara ya 58, kwa msisitizo ibara ya 59.
- Kitabu cha Kanuni za Uongozi na Maadili ya CCM na Jumuiya Zake, toleo 2022, ukurasa wa 2, ibara ya 4.
- The Political Parties Act, Chapter 258, inatutaka sisi kama chama cha siasa kuziishi kanuni, miongozo, na taratibu zetu bila kusubiri kusimamiwa na wengine.
- Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, toleo la 2005, ibara ya 26(1)(2), ibara ya 9(a, b, f, na h), na ibara ya 29(1)(2).
- Ilani ya CCM 2020, ukurasa wa 1, ibara ya 4, ukurasa wa 161-168, ukurasa wa 8, ibara ya 10 na 11.
"Integrity ni jambo muhimu sana. Ni vizuri hizi kanuni tuzisome. Sasa mnatakiwa kuziishi, sio kuzisoma tu, bali pia kuziishi na kuzitekeleza."
Mwisho wa kunukuu.
Tusome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, toleo la 2005, ukurasa wa 13, aya ya kwanza, na ibara ya 12(1)(2), ibara ya 13(1)(4)(5).
Nchi yetu itapiga hatua endapo tutajipa ujasiri wa kukemea adui ujinga, ambaye ndiye adui namba moja aletaye umasikini na maradhi.
Kila kukicha, ujinga unatufanya tuzidi kuwa wanyonge, na wanaopaswa kutupa elimu wamegundua njia pekee ya kutudhulumu ni kutumia makundi ya watu wajinga, kuyawalisha ubwabwa na kisha wajinga hao kujizima data na kushangilia lolote na chochote.
Huku majina mengi yakiwa na ujinga wa kutojua ilani, katiba, kanuni, miongozo, na taratibu za kimfumo, yanakubali kushiriki vitendo vya kipumbavu kwa ahadi ya ubwabwa. Badala ya kutafuta elimu na maarifa, yanashirikiana kumkejeli mtu anayejitahidi kuyasaidia kutoka kwenye dimbwi la ujinga.
Tuisome Katiba ya CCM ya mwaka 1977, toleo la 2022:
- Ukurasa wa 02-03, ibara ya 05(14)
- Ukurasa wa 06, ibara za 07, 08(1)(2)(6), na 15(3)(4)(6)(7)
- Ukurasa wa 07, ibara ya 12(1)(a)
- Ukurasa wa 152, vifungu vya 1, 3, 6, 8, na 9
Akiwa SUA, Morogoro, tarehe 07/05/2018, alisema:
"Tulikuwa tumejenga element ya kudanganya kila kitu. Sasa element hii ni lazima tuibadilishe katika maisha yetu. Sisi Watanzania tujifunze kusema ukweli."
Adui ujinga humwingia na kumuishi mtu bila kujali cheo au kipato. Ujinga upo kila sekta.
Akiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya uzinduzi wa Chuo cha Ufundi Stadi huko Kagera, tarehe 13/10/2022, alisema:
"Mwasisi wetu wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere, katika wakati wake alipigania uhuru wa nchi yetu. Na baada ya kupata uhuru, alisema mambo matatu makubwa: la kwanza ni njaa, lakini pia ujinga na maradhi. Mwalimu alisema hawa ni maadui watatu wakubwa wa Taifa letu, na katika wakati wake aliyafanyia kazi kwa kiasi kikubwa."
Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, tarehe 30/04/2014, alisema:"Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa analinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alikuwa anailinda katiba."
================================================
(Baadhi ya Viongozi) Wasitumie Mwalimu Kama Hirizi
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alichokuwa akisema, pia alikuwa anatenda. Hawa (baadhi ya viongozi) wanasema kimoja lakini wanatenda kinyume kabisa na jinsi ambavyo Mwalimu angefanya.
Ndani ya Nchi:Mheshimiwa Rais akishasema, sisi ni utekelezaji. Hata hivyo, tunashuhudia mambo ya kijinga. Watu wanapinda mifumo, wanapeana vyeo kiholela. Tunayaona, lakini kwa ujinga tunapewa vitisho, tunawachekea viongozi wasio stahili. Matokeo yake, tunaona watu hawasomi mapato na matumizi huku wakilindwa kwa gharama zote. Sisi wasema kweli, tunatengwa na kuwindwa.
Dkt. Damas Daniel Ndumbaro - Waziri wa Katiba na SheriaNakumbuka tarehe 12/10/2022 alisema:
Tunaletaje haya huku tukiwacha watu watuonee bila ya kuchukuliwa hatua? Tusome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Toleo 2005, Ibara ya 34(4) na Ibara ya 35(1).“Sheria ni jambo muhimu sana katika utawala bora. Ni jambo muhimu katika utawala wa sheria. Ni jambo muhimu katika kuleta amani na utulivu katika jamii.”
Kuwajibika Kama Wazalendo:Tunawezaje kujiita wazalendo ikiwa tuliapa kutokupendelea, lakini sasa tunapendelea watu mchana kweupe kana kwamba hatukuapa wala kushika vitabu vya Mwenyezi Mungu? Tumeshiriki kwa kiasi gani kuondoa mambo haya ya kijinga yanayokiuka viapo na kuviza haki za mafukara? Twawezaje kusema tuna akili ikiwa tunakiuka viapo vyetu na kisha kukimbilia kwa watumishi wa Mungu tukitaka kuombewa?
Mwalimu Nyerere Alisisitiza:Mwalimu alisema:
Baadhi ya Hoja Muhimu za Viongozi:“Ujinga, mtu akishaambiwa, inakwisha. Kwa sababu ujinga ni kutokujua. Sasa ukielezwa, ujinga wako unakwisha.”
- Hayati Rais Benjamin William Mkapa - Alisema ni muhimu kurejea falsafa za Mwalimu kuhusu kupambana na maadui watatu: umaskini, maradhi, na ujinga.
- Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli- Katika hafla mbalimbali alisisitiza:
- “Upumbavu kama huu siwezi kuwa mpole” (Masumbwe, 27/11/2019).
- “Tupambane na maadui wa maendeleo, na tujifunze kutoka kwa nyuki” (Rufiji, Julai 2019).
- Professor Abubakar Bin Zuber - Alisema Uislamu ni dini ya kwanza kupiga vita ujinga na dhuluma, na kutetea haki (14/10/2018).