Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
Inashangaza kuona taaluma ambayo pengine ingetakiwa kua msaada kwa taifa letu lakini imegeuka kua ni kichaka cha vioja. Kuna mdau alikuja kulalamika humu siku moja ya kwamba Baraza la famasia na Chama cha wafamasia wamejikita kwenye kufungia maduka ya watu na kujiwekea ubinafsi wa wao pekee kufanya biashara ya dawa badala ya kujikita kwenye taaluma yao na kulisaidia taifa.Sasa nimemuelewa huyo mdau humu.
KUHUSU TUKIO LA TURIANI MFAMASIA KUMNWESHA MGONJWA DAWA YA UPELE.
Tunaposema chama cha wafamasia na baraza la famasia badala ya kushughulika na matatizo ya watu wao wanajikita kwenye ugomvi na fani ziingine nani auze dawa na nani asiuze dawa, wanaacha mambo muhimu katika kusimamia taaluma ili kulinda afya za watanzania.
Haya, walizoea kusema manesi na madaktari kwenye maduka ya madawa ndio wanaotoa dawa kimakosa,je, huko TURIANI Morogoro ni daktari au Nesi ndiye aliyetoa dawa? Ilikuwaje Mwanafunzi ambaye amefundishwa na Mfamasia aliyefunzwa akaiva akamywesha mgonjwa dawa ya upele? Huyu anayeitwa Mwanafunzi wa famasia ilikuwaje akatoa dawa peke yake?
Alaumiwe nani hapa?
Kukosekana kwa umakini katika taaluma hii na kujikita kwenye maslahi binafsi ndiyo matatizo yake haya. Kitendo kilichofanyika kule TURIANI ni cha aibu na kinaonyesha jinsi ambavyo katika taifa letu tuna watu wa ajabu. Kumnywesha mgonjwa dawa ya Upele ni kesi ya jinai na sijui ni kwanini hili jambo linachukuliwa poa.