Nyie wafanyabiashara katika mgomo wa leo napenda kuwataarifu kwamba hamko pamoja, Nikijikita zaidi katika mji wa Kahama Shinyanga ni kweli maduka hapa centre hayajafunguliwa, lakini wafanyabiashara wengi tu wanawasiliana na wateja wao na biashara wanafanyiana nyumbani kwenye maghala. Bahati mbaya kuna baadhi ya wafanyabiashara kama wenye feremu za autospares, lubricants, cosmetics n.k hawana maghala naona mtaathirika zaidi kama mgomo utachukua muda mrefu.
Jaribuni kufikiria sababu dhumuni la mgomo hoja zake ni vigumu kuzitetea, yaani ukimweleza mtu bila chenga kabisa inaonekana ni ukwepaji wa kodi!!