Wafanya biashara Lipeni kodi acheni ubabaishaji

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
Zitto Kabwe

EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010 kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD, makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni. Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs 1,086 bilioni. Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63 mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara 16,000.

Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta (Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato inatarajia kukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake iwapo EFD zitatumika.
Wafanyabishara kote nchini wanalalamika. Mwanzoni hoja kubwa ilikuwa ni bei za mashine hizi. Hoja inayoeleweka kabisa. Kamati ya PAC iliwahi kushauri kuwa Wafanyabiashara wapewe bure kabisa mashine hizi (bila kusubiri kurejeshewa kupitia kodi. Kimsingi mashine hizi ni Bure isipokuwa Mfanyabiashara huikopesha TRA na TRA kumrudishia kupitia kodi ya Mapato katika mwaka wa kwanza wa matumizi).
Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?
Wafanyabiashara wanasema kodi ya VAT ya 18% ni kubwa mno na inakatwa bila kuzingatia manunuzi yao ie gharama zao za uzalishaji. Siku zote VAT inakatwa kutoka kwenye mauzo ghafi au kutoka faida?
Hebu tujadili masuala haya na yale malalamiko ya msingi yafanyiwe kazi na yasiyo ya msingi yapuuzwe.
Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba.........​





swala la kugoma kulipa kodi ni kutoitendea haki serikali,wafanya kazi tunalipa kodi ya kichwa-kodi ya mapato,tunalipa VAT,bado tunalipa kodi ktk vitu tunavyonunua.
wafanyabiashara acheni ubabaishaji,lipeni kodi kwa manufaa ya Taifa hili,huu si wakati wa kugomea hizo machine na mbona nchi nyingi tu wanatumia hizi machine? inakuwaje nyie hapa Tanzania mnaleta mgomo eti hamtaki kulipa kodi?
Hapana,wafanyabiashara lipeni kodi kwa maendeleo ya Taifa hili

mnapokwenda china kununua vitu,mnapewa risiti toka ktk vimeshine ambavyo hapa mnavigomea,lakini mkiwa china hamgomi kupokea risiti inayokuonyesha kodi kiasi gani umelipia toka ktk ile bidhaa uliyonunulia,mnaogopa kugoma mkija china kwani mnaelewa serikali ya china haiwezi kuwaonea huruma na itawang'oa shingo,lakini mnaporudi na mzigo Tanzania mnagomea machine hizo na tena pesa yenyewe inatoka kwa wanunuaji ndio wanaolipa kila aina ya kodi unayotakiwa kulipa.
Hapana lipeni kodi wafanyabiashara.
 
tena kodi kama vat hawalipi wao,wao ni mawakala tu wa kuikusanyia serikali,anaelipa ni mlaji wa mwisho.walipe wasitutanie kabisa hawa!
 
Ni UJAMBAZI MKUBWA, kodi analipa mlaji wao wameshazowea kuitia mfukoni bila kuiwasilisha TRA, sasa mwenye mali kaamua kubana wao wanalia kama vile ni haki yao!!!
 
Sidhani kama tatizo ni kodi tatizo ni mashine za kutolea kodi,kodi hata iweje mtumiaji wa mwisho atailipa tu ila ishu ni bei ya mashine za kutolea hzo risiti ndio haziendani na mfanyabiashara


Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Sidhani kama tatizo ni kodi tatizo ni mashine za kutolea kodi,kodi hata iweje mtumiaji wa mwisho atailipa tu ila ishu ni bei ya mashine za kutolea hzo risiti ndio haziendani na mfanyabiashara


Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Mkuu tatizo kubwa hapa ni gharama za ununuzi wa hizo mashine.. Mie nina duka langu ambalo mtaji wake ni milioni mbili.. Humo ndani nina muuzaji ambae analipwa.. Kuna kodi ya pango ambayo inalipwa.. kuna malipo ya TRA ya mwaka (ambayo minimum makadirio ni shilingi 290,000.. umeme ambao ni shilingi 60,000 kwa mwezi.. bado kuna ushuru wa uchafu ambao unatakiwa ulipe.. Juu ya yote hayo unakuja kupewa mzigo wa kununua mashine kwa shilingi 600,000..! Piga hesabu hapo uone kama kuna uwezo wa kununua hiyo mashine..

Ingekuwa ni vema wakatoa kwa mkopo mdogo ambao mfanyabiashara anaweza ku-afford kulipa.. Wangefanya hivyo ingeweza sana kusaidia kwa TRA na kwa mfanyabiashara pia..

NB: Hapa ninawazungumzia wafanyabiashara wadogo sio wale wakubwa ambao naona wameingilia kati na kulifanya hili ni la kwao..
 

sina uhakika....lakini nafikiri hio hela utakayotumia kununua EFD utarudishiwa kwenye kodi utakayolipa.....kama ulitakiwa uwakusanyie VAT laki nane utapeleka laki nane minus bei ya EFD.
 
tena kodi kama vat hawalipi wao,wao ni mawakala tu wa kuikusanyia serikali,anaelipa ni mlaji wa mwisho.walipe wasitutanie kabisa hawa!

Ni kweli kabisa,sisi walaji ndio walipaji wa hizo kodi na kama wangekuwa na huruma na walaji basi bei ya vitu wangeiweka chini,lakini wao wanauza vitu bei kubwa na wanapata faida kubwa lakini serikali ianpotaka kuchukua kodi iliyokuwa ikipotea wanajifanya kugoma,hii haikubaliki
Nipo china naelewa bei ya vitu na nimewahi safirisha bidhaa kuja Tanzania,hawa wafanyabiashara wanauza vitu vyao mala 3 hadi 4 ya bei waliyonunulia hapa na wanapata faida kubwa sana.
na ikumbukwe kuwa kama ulivyosema wao ni mawakala tu wa kukusanya kodi,ila kodi inalipwa na mlaji wa mwisho kabisa
 
Sidhani kama tatizo ni kodi tatizo ni mashine za kutolea kodi,kodi hata iweje mtumiaji wa mwisho atailipa tu ila ishu ni bei ya mashine za kutolea hzo risiti ndio haziendani na mfanyabiashara


Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Hapana tatizo si machine,tatizo ni wafanya biashara hawataki kulipa kodi ambayo wao si walipaji ni walaji wa mwisho ndio walipaji.
 

Acheni ubabaishaji wafanyabiashara,mnaleta siasa ktk jambo la msingi
Mlielezwa mpeleke mapato na matumizi ya kila mwaka,ili muweze kupewa mashine bure,lakini mkakataa kufanya hivyo eti kwa kuogopwa kukadiriwa kodi kubwa,lakini lengo ha;ikuwa kuwakadiria kodi,lengo lilikuwa ni kutaka kuelewa kwa mwaka unapata kiasi gani ili wahusika waweze kuwapa hizo mashine kwa lengo la kukusanya kodi,mkakimbia na kuanza kugoma eti bei ni kubwa
sawa bei ni kubwa lakini kwanini hamtaki kukaa meza moja na srikali mkaliongelea hilo? na mbona ktk vikao na TRA wafanyabiashara huwa hawaendi? lengo ni nini?
 

tatizo katika nchi yetu wafanyabiashara kwa muda mrefu wamekuwa hawalipi kodi kama jinsi inavyotakiwa, ndiyo maana kila mtu anakimbilia huko. huu ndiyo muda wa kujua nani ni mfanyabiashara wa kweli na nani ni mbabaishaji, Serikali kwa hili tupo nyuma yenu lazima walipe kodi mbona sisi wafanyakazi huwa hatubembelezwi kama hivi? hasa ukizingatia sisi wafanyakazi pamoja na kuwa mishahara yetu ni midogo lakini tunalipa kodi kubwa kuliko hata hao wafanya biashara.
 
sina uhakika....lakini nafikiri hio hela utakayotumia kununua EFD utarudishiwa kwenye kodi utakayolipa.....kama ulitakiwa uwakusanyie VAT laki nane utapeleka laki nane minus bei ya EFD.

Sasa kwenye hiyo business si umeona makadirio yake ya kodi ni 290,000 shs sasa inamana ndo hatolipa kodi mwisho wa mwaka kwa miaka miwili au vipi..kama TRA walitoa majibu ya hivyo obviously waliwalenga wafanya biashara wakubwa....!!
 
Sasa kwenye hiyo business si umeona makadirio yake ya kodi ni 290,000 shs sasa inamana ndo hatolipa kodi mwisho wa mwaka kwa miaka miwili au vipi..kama TRA walitoa majibu ya hivyo obviously waliwalenga wafanya biashara wakubwa....!!

Nashukuru Mkuu kwa kunielewa.. Tatizo la kwanza ambalo ninaliona hapa ni wafanyabiashara wote kuwekwa kwenye kapu moja.. Mie kwa upande wangu sina matatizo na hizo mashine zaid ya gharama zake.. Hamna mfanyabiashara mdogo ambae atakuwa na uwezo wa kununua hizo..
 

Ndio hivyo ndugu yangu

inauma sana unapoona siasa zinaingia hadi ktk mambo ambayo hayahitaji siasa
 

inavyosemekana ni kwamba hao wafanyabiashara wakubwa nao wamo,hawataki kutumia hizo machine ili kuweza kuisaidia serikali kukusanya kodi.
na sijawahi ona mfanyabiashara kuwa na huruma na mteja,mala zote wao wanakimbilia faida kubwa na utajiri,lakini serikali inapotaka kodi tena toka kwa walaji wa mwisho wao wanakuja na kujifanya wanahuruma na walaji
hapana,waache serikali ikusanye kodi.
huwa wakisikia mshahara umepanda na wao wanapandika bei ya vitu,bila kuelewa kuwa wafanya kazi wamebeba mzigo mkubwa sana ktk nchi hii,wanalipa kodi ya KICHWA ambayo imefutwa kwa wasiowafanyakazi na bado wananunua vitu na kuvilipia kodi,lakini wao wafanya biashara hawataki kuwa mawakala wa kukusanya kodi,kwani kiuhalisia wao si walipa kodi,kazi yao ni kukusanya tu.
 
Ni kweli wafanyabiashara si walipaji kodi. Mfanyakazi wa serikali wa kipato cha chini; analipa kodi kubwa zaidi ya mfanyabiashara mkubwa. Sisi hatusamehewi kodi mpaka kustaafu.
Binafsi naunga mkono hatua za serikali katika ukusanyaji wa kodi ambazo wafanyabiashara wamekuwa wanazikwapua toka kwa mtumiaji wa mwisho, lakini hawazipeleki panapostahili kwa kuwa hakuna kumbukumbu. Tatizo ni hizo mashine ziuzwe (hata ukisema watarudisha gharama, bado ni kuuza tu), au zigawiwe bure? Na kama ziuzwe, je zinauzwa kwa thamani halisi? Halafu sijajua hivi mtu akinunua leo, baada ya miezi kadhaa ikafa; atanunua nyingine au atapewa bure au ndio mambo ya warranty au guarantee yanaingia hapo?
 
Wafanyabiashara wakubwa walipe afu mishahara ya rais, wazr mkuu + wabunge nayo ipunguzwe hela zisaidie kujenga nchi
 
Jamani tatizo sio bei za efd machine ni kubwa nina uhakika hata ukiwapa bure hawatazitumia kabisa.tatizo lililopo ni mfumo tulionao wa kufanya biashara Tanzania.kwa ufupi kodi inayolipwa TRA si VAT yote bali ni jumla ya VAT ya mauzo utoe VAT ya manunuzi (au ile uliolipia mzigo bandarini) kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje na hapa ndio kuna shida kubwa sana.Bidhaa zinazoingia nchini nyingi zinapita Zanzibar na zinaingizwa nchini kupitia bandari bubu na kuingia kariakoo zikiwa hazijalipiwa ushuru wowote.Jiulize huyu mtu VAT ya manunuzi(purchase) ni zero maana yake anatakiwa alipe VAT 100% na hapo ndio kiini cha mgogoro.Tujiulize bidhaa zinafikaje kariakoo wakati TRA wapo na polisi wa Doria wapo?
Suala la pili ni bidhaa tunazonunua ndani ya nchi ambazo nazo hazipo kwenye mfumo wa kodi kama mazao ambayo mkulima anayauza na yenyewe yaongezewe VAT na mlaji yupo tayari kulipa?
Nakubaliana na wachangiaji kwamba wafanyabiashara wanapaswa kulipa hizo 18% na serikali nao inapaswa kukomesha uingiaji holela wa vitu katika mipaka yetu.Hali hii ikiendelea itawaadhiri sana investors hasa wenye biashara kama za watu wa kariakoo.
 

Asante mkuu kwa maelezo mazuri yenye kujenga
 

Wrong......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…