Wafanyabiadhara mnakera sana na bei zenu zisizoendana na uhalisia

flood

Senior Member
Joined
Jul 10, 2017
Posts
121
Reaction score
188
Leo naomba niongee na wafanyabiashara hasa hawa wa rejareja. Kuna hii tabia inaboa sana na inatufanya tusijiamini wakati wa kufanya manunuzi kama vile hukujiandaa maana ukijidai kupack kama vile uko Nakumati (sijui kama watarudi) unaweza ukaumbuka.

Kifupi ni kwamba unajua kabisa hiki kikombe ni Tsh 500 ila utaambiwa Tsh 2000 ukimuambia punguza atakuambia Tsh 1800 ukiondoka anakuita kwani wewe una shilingi ngapi?Ukimtajia anakuambia haifai ila mwisho atakuambia basi leta tu.

Hii tabia imenifanya nihamishie shopping zangu kwa wahindi na kiukweli hawa jamaa wanajua biashara kwanza bidhaa zao ni genuine zina ubora, upande wa bei vizuri sana na hata warrant zao ni za kuaminika.

Hebu tubadilike katika hili ukipata faida Tsh 200 na ukaletewa wateja wengine 10 utakuwa na faida ya Tsh 2000 kuliko kusubiri faida ya Tsh 500.
 
yes yes, hapo ni kweli kabisa...waTZ tatizo maneno mengii, wanasababisha hata mtu akiambiwa bei anajua tu hii lazima ni ya kuanzia tu.

wakati mwingine mtu ukiwa umechoka unaingia tu SM unaona bei unachukua unaenda kupumzika kuepuka wamachinga kuzozana naoo
 
Wa DAR linwahusu hili, ushaona wapi bei inapungua toka efu14 mpaka efu 5 kama sio wizi
Sijui wanawazaga nini mtu anaanzia 30000 unamwambia inatosha sina hiyo hela anashuka mwenyewe mpaka 10000 has a kkoo
 
Biashara hizo mwachie Dr.Shika we nenda kwa wahindi
Just kidding.
 
muuzaji anaweza kufanya price discrimination kutokana na mteja na mahali,tatizo wanakuwa walafi wanaweka bei kubwa sana na za ajabu begi la 20,000 anakwambia 60,000.
 
yes yes, hapo ni kweli kabisa...waTZ tatizo maneno mengii, wanasababisha hata mtu akiambiwa bei anajua tu hii lazima ni ya kuanzia tu.

wakati mwingine mtu ukiwa umechoka unaingia tu SM unaona bei unachukua unaenda kupumzika kuepuka wamachinga kuzozana naoo
Kuna kipindi nilikuwa na shida na simu ndogo, nikaenda kwenye maduka ya Tecno pale makoroboi..

Nimefika kwenye duka la kwanza nikakutana na mganda anauza huku simu zikiwa na price tag kabisa nikashika Tecno ya 25,000/= nikamuuliza vipi hakuna punguzo? Akasema bei nnayoiona ndio hiyo hiyo hakuna punguzo!

Nikasogea duka la pili nikamkuta dada flani mbongo nikashika Tecno kama ile ile niliyoishika kwenye duka la kwanza ilikuwa haina price tag nilipomuuliza bei akaniambia inauzwa 30,000/= nikamuuliza tofauti na hapo unauza shilingi ngapi? Akajibu kama nna nia ya kununua nimpe 28,000/=. Sikuendelea kukaa pale mimi nikaondoka wala sikumjibu swali lake alipuniuliza kwani wewe unashingapi.

Nipiga mizunguko yangu baadae nikaenda kwenye yale yale maduka safari hii niliingia kwenye duka lingine nikamkuta Mzee mmoja wa kipakistan alikuwa anauza simu ndogo zote bei moja ambayo ni 26,000/= kasoro Samsung, nikicheki mfukoni nna hela ndogo sana. Nikamua kuondoka nikaenda moja kwa moja kwenye lile duka la dada wa kibongo kwa sababu nilijua tu yule ana msimamo na bei ya bidhaa zake.

Kufika pale nikamwambia dada aniuzie ile simu niliyoishika muda mfupi uliopita lakini sio kwa ile bei anayoitaka yeye hela niliyo nayo mimi ni 20,000/=, akasema hauzi simu yoyote kwa hiyo bei, nikamuuliza bei ya mwisho shingapi!? Akasema nimpe 27,000/= tokazozana zozana pale mwisho nikwambia basi nakuongezea 2,000/= uniuzie kwa 22,000/= ikishindikana na hapo basi hii sio bahati yangu. Mara yeye mwenyewe akaanza kujishusha, basi leta nikuuzie kwa 25,000/=. Nikamwambia labda nikupe 23,000/=.

Niliichukua ile simu kwa 23,000/= kutoka initial price ya 30,000/=. Nilichokiona pale wabongo hatuna misimamo thabiti ya biashara, tunajifanya wajanja wajanja lakini tunaogopa loss, tofauti kabisa na wafanya biashara wa jamii zingine.
 
umeona ss....
hata siku nyingine ukienda utajua uanzaje!
 
Aisee hapo umeongea ukweli bwana na hilo ndilo lililo tusababisha watanzania wengi biashara zetu zishindwe kupanuka
 
umeona ss....
hata siku nyingine ukienda utajua uanzaje!

waswahili wanapenda sana kuleta majaribu ya bei kwenye biashara halafu ni waoga kupoteza wateja.

Na mimi nikiuziwa vitu na mswahili lazima tushushane tu, ni mara chache sana mswahili atakutajia exact price pale utakapomuuliza.
 
Hakuna wafanya biashara wanaopanga bei za ajabu kama wa maduka ya dawa na maduka ya nguo za watoto....utakuta dawa kwa bei ya jumla amenunua 2300 lkn yeye anauza 4000 au nguo ya mtoto ya kawaida kabisa eti inauzwa 60000 kweli!!!?wakati ukizunguzunguka k/koo nguo hiyohiyo unapata kwa 37000.
 
Back
Top Bottom