PLATO_
Senior Member
- Jan 25, 2020
- 116
- 230
Leo nimepita mitaa ya Mwanjelwa nimekuta fremu zimefungwa. Wamachinga wanaendelea na biashara zao kama kawaida.
====
Pia soma:
====
Ni siku ya pili ya muendelezo wa mgomo wa wafanyabiashara Jiji Mbeya, kutokufungua maduka waliodai hauna kikomo mpaka pale Serikali itakapotatua changamoto zao za kikodi.
Katika mitaa mbalimbali maarufu ya biashara Jijini humo hakuna huduma yeyote inayopatikana zaidi ya machinga wanaoendele na shughuli zao huku wakieleza changamoto wanayokumbana nayo kwa kukosa bidhaa ambazo wanategemea kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa ndipo waingie sokoni kuuza.
Chanzo: ITV
Pia soma: