Wafanyabiashara mtandaoni mkiweka bei za bidhaa zenu bayana mnapungukiwa nini?

Wafanyabiashara mtandaoni mkiweka bei za bidhaa zenu bayana mnapungukiwa nini?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Unaamua kufanya biashara mtandaoni halafu huweki bei, lengo lako ni nini?

Inakera sana unakuta ukurasa umejaa watu wanauliza bei halafu hazijibiwi au wakijibu ni jibu la 'njoo DM' au 'piga namba hiyo hapo' ama 'kwa maelezo zaidi njoo WhatsApp'.

Kwani mkiweka bei kila mtu akaona mnapungukiwa nini? Tena si ndio inarahisisha mtu anajipimia mwenyewe kama anawezana nacho ama atarudi siku nyingine?

Acheni mambo zenu bana, mnakera sana!
 
Utatajiwa bei jinsi utakavyokuja, kiufupi kila mteja na bei yake!!
 
Utatajiwa bei jinsi utakavyokuja, kiufupi kila mteja na bei yake!!
Hii haiko sawa. Unakuta mtu pia anatangaza promotion au mambo ya betting anasema jishindie Hadi milioni ishirini.

Huu ni upotoshaji mwingine Kwa sababu huwezi ukawa unashinda bahati nasibu/kamari wewe peke yako Kila siku.

Kuna matangazo huko redioni mtu Hana ada ya shule ya mtoto anaambiwa akacheze kamari atapata Hela ya ada. Hivi tunaelekea wapi?
 
Back
Top Bottom