Wafanyabiashara na kutosomea customer Service

RGforever

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
6,878
Reaction score
5,432
Kuna Baadhi ya watu kumbe umasikini sometimes upo kwenye damu .. Hebu Angalia haya majibizano kati ya muuzaji wa magari na mteja.. Gari ilikuwa inauzwa Mil 7(fixed) kaandika muuzaji wateja wakakomment..

Sasa Muuzaji hivi unategemea utapata wateja kweli kwa majibu ya Hivyo..
 
Daaaah ni kweli javisa hii kituvinatufelisha wengi sana asee
 
Kwake yeye Mteja si Mfalme.

Biashara inabidi uwe mpole ili kumshawishi Mteja wako.

Sasa kauli nzito kama hizo "Pita kushoto"!

Kwa Mteja mwenye NIA ya kweli ujue hapo unamfukuza
 
Kwake yeye Mteja si Mfalme.

Biashara inabidi uwe mpole ili kumshawishi Mteja wako.

Sasa kauli nzito kama hizo "Pita kushoto"!

Kwa Mteja mwenye NIA ya kweli ujue hapo unamfukuza
Kuna wateja huwa wapo wana view product silently hawacomment ila wanasoma tu... Sasa wakikutana na kauli hizo ..

Watahisi hata ni tapeli
 
Huwa nashangaa pale mfanyabiashara anapomjibu mteja 'ww mteja mmoja hunipunguzii chochote' huwa najiuliza huyo mteja akienda kusambaza 'negative words' khs hiyo biashara ni kweli hatompunguzia chochote au wanashindwa kufikiria madhara ya baadae
 
Hata humu tazama mtu anahza kiwanja Salasala
Majibu anayotoaga huwa ni kama haya.
 
Sio wote mbona kama mm nina customer care
 
Sio wote mbona kama mm nina customer care
Ni baadhi tu..
Ila kwa Tanzania customer care ipo hotelini na wale wamama wauza mihogo na nazi

Kwingine hakuna kitu.

Ndio maana wafanyabiashara wengi wanakufa njaa.
 
Kauli mbaya hupelekea kupoteza wateja ...
 
Bongo customer care ipo kwenye kutongoza tu sio sehemu nyingine

Jana nilikuwa sehemu nanunua kifaa fulani sasa nikaanza kuomba jamaa anipunguzie bei nikamtajia ambayo nipo willing kulipa jamaa akanijibu '... Kwa bei hiyo kama ni kuuza ungekuta mzigo umeisha Na nimeenda kuchukua Mwingine ...' Kwa kweli nilishindwa kujizuia kucheka
Yaan Watu Muda wote Ni visirani tu
 
Mbona wengine tushazoea, tunanunuaga tu sababu hatuna option nyingine, yaani wabongo wengi customer care ni sifuri kabisa, Hakuna kitu kabisa.
 
Wabongo wachache sana wako serious na biashara , wengine wamejikuta tu wako humo, unakuta Customer care mbovu na kupenda kupata super profit kwa muda mfupi, wakati kina muda unatakiwa kupata faida kidogo ili ujenge wigo mpana wa wateja pamoja na imani kwa wateja wako , waliosema biashara ni imani hawakuwa wapumbavu.
 
haha tusiwalaumu sana TRA imewavuruga sana
 
Kuna Wateja wengine pasua kichwa kweli kweli, ukikutana nao unaweza tamani kuacha hiyo biashara.. [emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…