Wafanyabiashara na wakulima wa Tanzania Usafi ni muhimu

Wafanyabiashara na wakulima wa Tanzania Usafi ni muhimu

Mr. Marangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,574
Reaction score
1,549
Kuna jambo moja haliko sawakwenye biashara za mazao ya kilimo, Bidhaa mbalimbali zinazotoka kwa wakulima kwenda sokoni/mlaji, zinawafikia walaji zikiwa katika hali ya uchafu kwa mfano Tangawizi unkuta ina udongo ... Udongo mpaka inapoteza mvuto, ndizi mbivu zina uchafu ulioshikamana, Maharagwe yana uchafu mawe manyasi n.k.

Katika hali hiyo kuna mambo binafsi nimeyabaini kuhusiana na uchafu kuendele kuwepo kwenye bidhaa za kilimo.

Mosi baadhi ya wakulima wanauza bidhaa zikiwa katika hali ya uchafu kwakutokujua umuhimu wakuuza bidhaa zikiwa safi ama wengine wanauza zikiwa katika hali ya uchafu kwakufanya makusudi.

Chakushangaza baadhi ya hawa wafanya biashara wanatumia mikopo waliokopa Halmashauri ama kwenye taasisi za fedha elimu ya ujasiriamali wamepewa ila wanaamua kukaza fuvu. Swali ni je wanafanikiwa kulipa mikopo kwa wakati kwa wao kuuza bidhaa zikiwa katika hali ya uchafu?

Pili kuna baadhi ya wafanya biashara wanauziwa bidhaa zikiwa katika hali nzuri na usafi lakini wanaamua kuongezea uchafu ili kufanya ujazo uwe mwingi mfano kwenyemaharage wanaongeza vumbi,kwenye dagaa wanaongeza vumbi kwenye mchele wanaongeza chenga za mchele.

Rai yangu Maafisa maendeleo, watendjai wavijiji wasichoke kuwaelimisha umuhimu wakulima kwani kwasasa soko la bdidhaa za kilimo nikubwa nchi zinazotuzunguka wanatutegemea sana.

Pili wafanya biashara waache hujumu za kuchafua bidhaa hizo wanaua soko la ndani na la nnje , pia wanaweza kusababisha maradhi kwa watumiaji.
 
Back
Top Bottom