Wafanyabiashara Ngara walia na mifumo ya kodi Mipakani wamweleza Waziri Mkuu Majaliwa

Wafanyabiashara Ngara walia na mifumo ya kodi Mipakani wamweleza Waziri Mkuu Majaliwa

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Malalamiko ya mifumo ya kikodi maeneo ya mipakani kutokuwa rafiki, kumewasukuma wafanyabiashara wilayani Ngara, mkoani Kagera kuwasilisha kero hiyo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa bungeni, jijini Dodoma.

Baada ya kukutana na wafanyabiashara hao, Waziri Mkuu ameagiza Waziri wa Viwanda na Biashara kutuma timu ya wataalamu kwenda wilayani humo kuona jinsi ya kutatua kero hizo.

Wafanyabiashara hao pamoja na mambo mengine, wanalalamika kitendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutotoa elimu ya kutosha juu ya mifumo hiyo na badala yake wamekuwa wakiwatoza faini kwa makosa ambayo bado uelewa wao ni mdogo.

Soma Pia: Wafanyabiashara wa Ngara Watembelea Bungeni, Wakutana na Jafo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

 
Back
Top Bottom