Wafanyabiashara soko dogo Kariakoo wagoma kupisha ujenzi

Wafanyabiashara soko dogo Kariakoo wagoma kupisha ujenzi

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Dar es Salaam. Wakati mkandarasi wa kujenga soko dogo la Kariakoo na kukarabati lile kubwa lililoungua na moto akiwa amekabidhiwa mkataba wa kuanza kazi rasmi, wafanyabiashara katika soko dogo wametoa masimamo wao wa kutoondoka sokoni hapo.

Makabidhiano ya kuanza ujenzi kati ya mkandarasi ambaye ni Estim, yalifanyika leo Desemba 24 sokoni hapo kati ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam, Hassan Rugwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Estim, Bashir Jushmy.

Mwananchi iliyokuwa eneo hilo, ilishuhudia makabidhiano hayo,huku yakishuhudiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri na watendaji wengine kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Wakala wa barabara Vijijini na Mjini (Tarura).

Hata hivyo katika makabidhiano hayo hakukuwepo na uwakilishi wowote kutoka upande wa wafanyabiashara,sio wa soko lililoungua wala soko hili dogo.

Wakati wafanyabiashara hao wakiweka msimamo huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija, amesema ni lazma wahame na watawahamishia soko la Kisutu na lile la Machinga Complex.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Hussein Magaeli amesema wameshangaa kuona mkandarasi akikabidhiwa kuanza kazi wakati kikao cha cha juzi kati yao na Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla walikubaliana kuwa wafanye mazugumzo kwanza na Mkuu wa Wilaya kuhusia na utekelezaji wa mradi huo utakavyokuwa bila kuathiri biashara zao.

"Mazungumzo yetu kati ya mkuu wa Wilaya yalikuwa pamoja na mambo mengi tujue nmna gani tutaondoka hapa na vipi tutarudi,hivyo kwa hatua hiyo ni wazi kwamba tumepuuzwa na serikali ya mkoa kuamua kufanya inavyoona," amesema Magaeli.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa uhamaji katika eneo hilo unatakiwa uwe wa kimaandishi na sio kwa kusema tu kwa mdomo ambapo baadaye wataweza kukosa ushahidi na eneo lao kupewa watu wegine.

Kwa upande wake mfanyabiashara Angeline Agustino, amesema kuondolewa bila utaratibu sokoni hapo ni kutaka kuwarudisha wanawake kwenye shughuli zisizo halali.

"Hapa sokoni kumesititiri wanaake wengi wakiwemo wajane na qale qaliokuwa wanafanya shughuli zisizo halili zikiwemo za kuuza miili,sasa leo kuambiwa tunatakiwa tuondoke, pasipokujua tunaelekea wapi ni kuwarudisha wanawake kulekule," amesema Angelina.

Mwishehe Dizeru, ambaye ni msemaji wafanyabiashara hao, amesema katika utekelezaji wa mradi huo wanaona wanaendelea kutengwa kwani mbali na kilichofanyika jana cha mkandarasi kukabidhiwa kazi bila wao kuwepo.

Akijibu hoja hizo, DC Ludigija amesema mazungumzo na wafanyabiashara hao anatarajia kuyafanya Jumatatu na kuingoza kuwa suala la kuandikishiana pia liko kwenye mchakato, kwa kuwa lengo la mradi huo ni kuona wafanyabiashara wengi wanachukuliwa kuliko ilivyo sasa.

Hata hivyo, kiongozi huyu alibainisha kuwa wana taarifa kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara sokoni hapi wanapinga kuhama hapo na kuwahamasisha wengine kutokana na kuwa na vizimba zaidi ya kimoja ambapi wanawakodishia wengine, hivyo wanajua wazi wakaondolewa na kurudishwa watavikosa vizba hivyo.

Source: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amos Makala jana alisema hivi ila leo mwandishi wa Mwananchi anasema kamuhoji kiongozi wa wafanyabiashara na wamezungumza hivo.
millardayo_1640364603261.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwako muanzisha uzi huu kwa chanzo cha habari ulikoitoa ila iko hivi;

Kwanza kabisa Mama hajui kuhusu wafanyabiashara hao wa soko wadogo, anachojua ni kuwa soko la Kariakoo lote liliungua na linatakiwa lijengwe upya(kuna upigaji mkubwa mno wa kodi za hawa wafanya biashara wa soko dogo na hawana pa kulalamikia)

Pili, hawa jamaa waliletewa notice ya siku 30 tangu tarehe 01/11/2021 kuwa ifikapo tarehe 31/12/2021 wote wanatakiwa kuhamia eneo la Kigiragira ili watakapomaliza soko warejeshwe, hapa wafanyabiashara hawa akili ikawastuka kidogo. Tuhamishiwe kule bila utaratibu wowote rasmi halafu huku tutarudije!? Wakawa wameandika barua kwenda kwa Waziri wa Viwanda majibu yakarudi ya kihuni, wakamwandikia PM, haikujibiwa.

Tatu, waliomba wapewe soko kubwa ambapo waliwaambia watumwa na serikali ya kuwa, wamalize marekebisho ya soko kubwa, ili wao wahamie kule halafu likiisha kujengwa hilo linalotarajiwa, watarudi. Watumwa serekale wakakataa wakawaambia wameandaliwa eneo Kigilagila waende kule.

Nne, leo hii nilipita soko dogo kuchukua mahitaji ya ofisini kwangu, nikawa nazungumza na mfanyabiashara mmoja akawa amenipa jambo jipya kabisa, nikaielewa hii sarakasi inayofanywa na hawa akina Makalla na wenzie, binafsi nilichoka! Lile eneo limeshachukuliwa na Mkwere na GSM wanataka kudondosha Mall ya kucheba hapo mjini Daslam ndio maana kila kitu kinafanywa kwa force.

Alikuja Makalla juzi kuzungumza nao ila hawakufikia muafaka akayakimbia maswali akawaambia atakuja mkuu wa Wilaya ya Ilala azungumze nao nikajisemea wtf! Yaan umeshindwa kulibeba wewe mkuu wa kaya unakuja kumsusia kaa la moto mtu wa chini!? Wacha tuendelee kulitazama picha hili.
 
Hongera kwako muanzisha uzi huu kwa chanzo cha habari ulikoitoa ila iko hivi;

Kwanza kabisa Mama hajui kuhusu wafanyabiashara hao wa soko wadogo, anachojua ni kuwa soko la Kariakoo lote liliungua na linatakiwa lijengwe upya(kuna upigaji mkubwa mno wa kodi za hawa wafanya biashara wa soko dogo na hawana pa kulalamikia)
Wamekwambia pia wengine wamejimilikisha Vizimba zaidi ya Kimoja (Nje ya taratibu) na wanawalipisha wenzao gharama ya Pango ikiwa kubwa kuliko inayolipwa..!?
 
Wamekwambia pia wengine wamejimilikisha Vizimba zaidi ya Kimoja (Nje ya taratibu) na wanawalipisha wenzao gharama ya Pango ikiwa kubwa kuliko inayolipwa..!?
Inaweza ikawa pia au ikawa sinema. Nataka nikupe scenario hii ndogo sana kama utaweza kuitafutia majibu utayaleta. Angalia zile frem zilizojengwa pembeni ya soko dogo upande wa ubavuni ukiwa unakwenda Tahfif (mimi ni mbovu mno wa mitaa ya Kkoo miaka yangu yote hapa mjini) uliza wale jamaa wanalipa sh ngapi na kodi rasmi ni kiasi gani, kuna wale waliokuwa wana vifrem ubavuni mwa soko lililoungua, uliza wale walikuwa wanalipa sh ngapi per kila kijimlango, uliza wale waliowekewa bati katikati ya soko kubwa na soko dogo walikuwa wanalipa sh ngapi na uhalali wao wa kuwa pale. Pale mjini kuna ushenzi mwingi mno unafanyika na mind you, haikupita hata miezi miwili tangu Mama atoke pale sokoni likaungua. Think twice mzee.
 
Hongera kwako muanzisha uzi huu kwa chanzo cha habari ulikoitoa ila iko hivi;

Kwanza kabisa Mama hajui kuhusu wafanyabiashara hao wa soko wadogo, anachojua ni kuwa soko la Kariakoo lote liliungua na linatakiwa lijengwe upya(kuna upigaji mkubwa mno wa kodi za hawa wafanya biashara wa soko dogo na hawana pa kulalamikia)
Hii kitu hata mimi nimeshaisikia pia. Si ajabu watu wanadai nchi inaongozwa na mkwere kwa kutumia rimoti yaani huyo bibi hapo magogoni.
 
Back
Top Bottom