Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Licha ya Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa zaidi ya mwaka mmoja kubainisha wazi mpango wa ujenzi wa Soko la kisasa eneo la katikati ya Mji ambapo lipo soko ambalo limekuwa likitumika muda mrefu, lakini Wafanyabiashara ndani ya soko hilo walipewa taarifa ndani ya wiki mbili kwamba wawe wameondoka eneo hilo kupisha shughuli za ujenzi huo.
Taarifa hiyo ambayo ilitolewa kwenye kikao baina viongozi ikiwemo Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Steven Byabato na Wafanyabiashara wa Soko hilo, Desemba 18, 2024, walipewa maelekezo kuwa wawe wameondoka kwenye soko hilo ifikapo Januari 1, 2025 jambo limeleta gumzo.
Hata hivyo suala hilo limekuwa changamoto kwa Wafanyabiashara wengi kwa kutoliunga mkono suala hilo kutokana na kupewa muda machache wa kuondoka, pia licha ya hivyo wanaambiwa wahamie kwenye eneo la Baniani lililopo Nshambya kando na Mji huo.
Kichosikitisha zaidi licha ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa kuelekeza wahusika kuandaa eneo maalumu kama soko mbadala kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kibiashara kuendelea, pamoja na kuwezesha Serikali kuendelea kuingiza kipato.
Pamoja na kauli hiyo, kinachofanyika sasa mamlaka zinazoratibu suala hilo zinawaelekeza Wafanyabiashara kwenda eneo wanalodai ni mbadala Nshambya wajijegee wao miundombinu.
Suala hili linawaweka kwenye hofu ya kupoteza mitaji yao na kusababisha Serikali kukosa mapato ikizingatiwa eneo hilo sio rafiki kufika kwa kuwa lipo pembezoni ya Mji lakini pia utaratibu wa kutaka Wafanyabiashara wenyewe kujijengea miundombinu ni changamoto.
Wanapoanza kujijengea wenyewe inamaanisha mitaji yao ianze kutumika kuweka miundombinu mizuri wakati huo Serikali je, nayo itaweka vipi utaratibu wa kukusanya mapato au ndio itaacha kwanza ili Wafanyabiashara warejeshe kile wakichokitumia wakati wa maboresho ya Miundombinu?
Wito wangu kwa Serikali kupitia TAMISEMI ifuatilie kwa ukaribu suala hilo kwa kuhakikisha ujenzi wa soko hilo unafanyika bila kuathiri mitaji ya Wafanyabiashara.
Ni vyema mamlaka zinazoratibu suala hilo kuandaa miundombinu rafiki sehemu ambayo itafanya biashara kuwa endelevu bila kutegemea Wafanyabiashara wenyewe kujiandalia sehemu hizo jambo ambalo linaweza kuwa chanzo cha anguko kwenye biashara.
Itakumbukwa soko hilo linatarajiwa kujengwa kupitia Mradi wa uboreshaji wa Miundombinu Mbinu ya Miji ya Tanzania (TACTIC), sasa ni zaidi ya mwaka tangu mpango huo ulipobainishwa, lakini taarifa haikutolewa kwa Wafanyabiashara, sasa wanakuja kuwakurupusha wahame.
Pia soma ~ Mbunge Bukoba Mjini: Bilioni 47 kutumika ujenzi wa soko kuu la kisasa la Manispaa ya Bukoba