Wafanyabiashara soko la Kariakoo kuanza kurejeshwa Februari 2025, 336 wanadaiwa

Wafanyabiashara soko la Kariakoo kuanza kurejeshwa Februari 2025, 336 wanadaiwa

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema zoezi la kuwarejesha wafanyabiashara kwenye soko la Kariakoo lililopata ajali ya moto Julai 10, 2021 na kusababisha wafanyabiashara hao kuondolewa na shughuli kusimama, linatarajiwa kuanza mapema Februari mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Januari 29, 2025 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Hawa Ghasia amesema hatua hiyo ni kufuatia uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo, baada ya kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa soko, sambamba na kukamilika kwa kazi ya uhakiki wa waliokuwa wafanyabiashara kwenye soko hilo, uliofanywa na Timu Maalum iliyoundwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikijumuisha wawakilishi wa Wafanyabiashara, Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na vyomba vya Usalama.

Soma pia: Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024

Amesema kuwa Menejimenti inaratibu kazi ya kutangaza majina ya waliokuwa wafanyabiashara kwenye Soko hilo ambao wamekidhi vigezo na sifa za kurejeshwa baada ya uhakiki, ambapo Uhakiki uliofanywa umebaini jumla ya wafanyabiashara1,520 wanaotarajiwa kurejeshwa sokoni, huku Majina na fomu ya kujiunga yakitarajiwa kwa umma kupitia vyombo vya habari ikiwemo tovuti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na tovuti ya OR - TAMISEMI.

Aidha, Bi. Hawa Ghasia ametoa wito kwa Wafanyabiashara wote wenye madeni ya awali kabla ya soko hilo kuungua kulipa madeni yao kabla ya kurejea Sokoni, huku akieleza kuwa takwimu zinaonyesha takribani wafanyabiashara 366 wanadaiwa na Shirika hilo jumla ya Shilingi 358,571,106.85.

 
Back
Top Bottom