Wafanyabiashara stendi ya Mlowo Songwe waomba stendi ipewe jina la Daniel Chongolo ili kumuenzi

Wafanyabiashara stendi ya Mlowo Songwe waomba stendi ipewe jina la Daniel Chongolo ili kumuenzi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wananchi na wafanyabiashara wa stendi mabasi ya Mlowo wamekoshwa na hatua za utekelezaji wa umaliziaji uliokuwa ukisua sua muda mrefu wa vibanda na miundo mbinu yake.

Wafanyabiashara hao, kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na Mkuu wa Mkoa aliopo sasa Mkoani Songwe, Daniel Chongolo, wamependeleza kituo hicho mpaka kuanza kutumika kwa stendi hiyo. Hivyo basi, wameomba kituo hicho kipewe jina la Stendi ya Mabasi ya Chongolo.

Wakipiga stori na Habari Jamii Tz, wamesema itakuwa busara na zawadi ya pekee kwa Chongolo kupewa jina la stendi hiyo, ikiwa kama shukrani kwao, Wanasongwe, kwake.

"Tumeona halmashauri mbalimbali Mkoani Songwe zikizipa shule majina ya Wakuu wa Wilaya, au wakurungezi, wabunge na wenyeviti wa Halmashauri. Nasi tunaiomba Halmashauri yetu ya mbozi stendi hii ya mlowo ipewe jina la chongolo ili kumuenzi kwa juhudi zake alizozifanya hapa."
Michael Punde, mfanyabiashara Machinga


Wafanyabiashara hao wamekwenda mbali zaidi kuwa bila Chongolo, stendi hiyo isingefanya kazi, kwani maagizo aliyatoa na usikivu wa Halmashauri ya mbozi ndio yamepelelekea stendi hiyo kuanza kutumika kwa kasi.

Imekuwa ni desturi ya halmashauri nyingi Tanzania kuwapa majina viongozi wenye mchango mzuri kwa Wananchi, kama vile kuwapa majina ya shule na maeneo mengine, hivyo kumuenzi kiongozi huyo kama alama ya kukumbukwa.
Screenshot 2025-03-04 145156.png
Screenshot 2025-03-04 145030.png
Screenshot 2025-03-04 145050.png
Screenshot 2025-03-04 145140.png
 
Back
Top Bottom