Wafanyabiashara Tanzania wanalamba asali tamu

Wafanyabiashara Tanzania wanalamba asali tamu

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Haijawahi kutokea na haitakaa itokeee free ride kama waliyonayo wafanyabishara wa Tanzania kwa sasa, usishangae leo ukakuta sabuni ya kuogea inauzwa 500 kesho asubuhi ni 1200 ukilalamika unaambiwa ni vita ya ukraine

Rais wa nchi kama mara tatu kwenye hotuba zake amekuwa akisisitiza kwamba ni lazima bidhaa zipande ni kama vile alikuwa anawashangaa wafanyabishara kwa nini hawapandishi bei nao kiukweli hawajamuangusha maana neno la Rais ni amri wanaupiga mwingii sana

Bidhaa hazishikiki, moto unawaka kwelikweli si mchezo waliohamasisha bei zipande huko waliko wanafurahi sana maana hata bei ya nyama inapanda sababu ya vita vya ukraine

Haya bana hewala siye mafala tunashukuru wafanyabishara endeleeni kulamba asali ,huu wakati wengu mmepewa green light gongesheni bei hadi watu waite maji MMA
 
Ishauri Serikali ifungue Maduka ya Ujamaa upange foleni hadi jioni uambulie patupu.
 
Endeleeni kuimba mama anaupiga mwingi sana, mnanyooka sasa
 
Back
Top Bottom