Wafanyabiashara tujifunze kupitia haya majanga ya moto

Swahili AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2016
Posts
10,174
Reaction score
89,364
Habarini wana JF,

Kwanza kabisa nitoe pole kwa wafanyabiashara wote wa Soko la Karume, pamoja na Kariakoo (hawa sijawahi kuwapa kutokana na janga la moto walilopata).

Kuna suala moja ningependa tujifunze kupitia majanga kama haya ambapo yakitokea yanasababisha hasara kubwa kutokana na upotevu mkubwa wa mali unaotokea baada ya majanga hayo.

Kuna desturi ambazo tunazifanya kila siku ambapo punde majanga yatokeapo tunakuwa hatuna mahala pa kukimbilia na kuponyeshwa maumivu ya upotevu wa mali.

Mosi, KUNUNUA BIDHAA BILA KUDAI/KUCHUKUA RISITI na KUTOKUWA NA UTARATIBU WA KUWEKA KUMBUKUMBU

Hili ni tatizo kubwa kwa nchi, tunaponunua mizigo hatuchukui au kudai risiti. Nini hasara ya hili?

Kutokua na takwimu sahihi za mali tulizopoteza na kubaki kuumia ndani kwa ndani bila kujua kiasi tulichopoteza.

Kutokana na mazingira ya biashara watu wengi hawaweki kumbukumbu za mauzo, hivyo inakuwa ngumu kutambua mzunguko wa bidhaa ambazo muuzaji anauza.

Pili, KUTOKUWA NA BIMA ZA MAJANGA

Majanga kama haya yatokeapo, tunarudi nyuma kwa kiasi Fulani kutokana na upotevu wa mali uliotokea, sasa ni wapi pa kudai fidia? Kwa haraka tu, kama wafanyabiashara wangekuwa na bima juu ya biashara zao na majengo basi mau,ivu yao yangepoa kutokana na malipo toka mashirika ya bima ambapo mfanyabiashara anakuwa na dhamana nao.




 
Ushauri mzuri ila napenda niongezee kua,mamlaka husika zipitie haya Masoko na kuangalia safety standard,sio karibu na kibanda cha nguo unakuta Mama lishe nae anapika hapo hapo! au akimaliza shughuli zake hauzimi moto anauacha hivyo hivyo,hii ni hatari sana,

Pia issue za kuunganisha umeme kwenye hivyo vibanda ifanywe na wataalamu walioidhinishwa kufanya kazi hizo, kisha kue na ma inspectors wa kukagua kabla ya kuruhusu umeme kuanza kufanya kazi kwenye kibanda husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…