Wafanyabiashara wa Karikakoo watoa msaada Wa milioni 8 Gongolamboto

Wafanyabiashara wa Karikakoo watoa msaada Wa milioni 8 Gongolamboto

elimsihi

Member
Joined
Jun 30, 2024
Posts
5
Reaction score
5
Kikundi cha wafanyabiashara wanawake wa Karikakoo kinachojulikana kama Matumaini Mapya, kimekabidhi msaada wa viti 120 vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 8 katika kanisa la kipentekoste la Elbethel. Tukio hilo lilifanyika siku ya 7/7/2024 kanisani hapo Moshi Bar, Gongolamboto kwenye ibada ya shukrani iliyoendeshwa na Mch. Raphael Mhagama.

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Ndg. Theresia Kibona alitoa zawadi kwa baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakati alipokabidhi msaada huo wa viti kwa uongozi wa kanisa hilo pamoja na kuwashukuru Mch. Raphael Mhagama na mkewe Mch. Catherine Mhagama. "Kwenye shukrani kuna siri kubwa sana iliyojificha" —alisema Theresia Kibona wakati akishukuru kwa waumini wa kanisa hilo.

Aidha, Mch. Raphael Mhagama alisema kikundi hicho kimekuwa baraka kwao kwa kutoa msaada wa shukrani ya viti na zawadi kwa watoto yatima na wanawake wajane kanisani hapo. "Wametoa shukrani ya viti pamoja na vitu mbalimbali kwa wamama na wanawake waliofiwa na waume zao na watoto yatima pia." Akiongezea, alisema kanisa hilo limekuwa likitoa misaada ya kijamii hasa mahospitalini.

Pia, ametoa wito wa watu wenye pesa kuweza kushiriki katika kutoa misaada kwa jamii hususani kwa watu wenye uhitaji na waishio katika mazingira magumu. Kanisa hilo limekuwa likitoa misaada kama chakula, sabuni, mafuta na kujenga nyumba kwa jamii zenye uhitaji kwa miaka mingi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013.


IMG-20240713-WA0014.jpg

Pichani ni msaada wa viti vilivyotolewa na kikundi cha Matumaini Mapya kwa kanisa la Elbethel.
 
Mungu atawabariki sana kwa zawadi nzuri ya viti waliyotoa kwa mama kanisa
 
Back
Top Bottom