RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara - 38:
Baada ya kumaliza matembezi yangu kwa takribani wiki mbili kule jijini Mbeya. Leo nimefika Dar es salaam hivyo naomba niwashauri wafanyabiashara (wawekezaji) wakubwa wa kule Mbeya.
Wafanyabiashara wa Mbeya aamkeni;-
Mfanyabiashara wa Mbeya anafanya uwekezaji wa zaidi ya shilingi bilioni moja lakini watu anaowaajiri ni vijana waliokimbia umande.
Kwa mfano anajenga hoteli ya kisasa (uwekezaji wa zaidi ya bilioni 1) lakini Manager wa hoteli na wahudumu anaowaajiri ni wale vijana wa mtaani wasiojua "kusoma na kuandika" ili awe anawalipa mshahara wa Tsh elfu sabini kwa mwezi.
Uwekezaji wa zaidi ya Bilioni moja unamuweka Manager na wahudumu ambao hawajui kusoma na kuandika, wanajua kuongea kinyakyusa na kisafwa tu. Baada ya miaka 3 hoteli inadoda.
Ngoja niwaume sikio wafanyabiashara wa Mbeya;
Wafanyabiashara wenzenu wanapiga hatua ya kimaendeleo kwa sababu wanapowekeza mitaji mikubwa kama vile kujenga viwanda, makampuni, hoteli za kisasa, n.k - kwenye vitengo maalum wanaajiri watu wafuatao...
1. Watu ambao wataumiza akili.
2. Watu ambao watafanya tafiti za kutosha za kibiashara.
3. Watu ambao watamsaidia tajiri kutafuta masoko na kukuza biashara.
4. Watu ambao watakusanya data na kuzichakata kisha watakaa mezani na tajiri kwa ajili ya kufanya maamuzi mazuri ya kibiashara.
Baada ya miaka kadhaa unaona mabadiliko makubwa yanatokea. Wafanyabiashara wa Mbeya acheni kuokota vijana wa mtaani kisha mnawaweka kwenye vitengo maalum, wekeni (ajiri) watu watakaoweza kuwasaidia kwenye biashara zenu.
Right Marker
Dar es salaam