Wafanyabiashara wa migahawa huwa wanapataje faida wakiwa na rundo la wafanyakazi?

Wafanyabiashara wa migahawa huwa wanapataje faida wakiwa na rundo la wafanyakazi?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Katika biashara ya migahawa mingi huwa naona rundo la wafanyakazi ukilinganisha na ukubwa wa mgahawa.

Kuna mgahawa nimeona una viti 40 na wafanyakazi kama 30 hivi, kuna migahawa midogo midogo ya mtaani mingi ambayo haiwezi hata kukaa zaidi ya watu 5 lakini wafanyakazi wako 5!

Ninachojiuliza mmiliki huwa anagawanyaje mapato kumpatia kila mfanyakazi ujira wake na yeye abakie na faida ya maana pamoja na mtaji wa kuendeleza biashara!
 
Wanalipwa hela ndogo sana hao!! Biashara ya chakula inalipa sana mkuu, kilo moja unatoa sahani hata 10, sahani moja ya wali ni Tsh 2000 hadi 3000 inategemea na mboga yake... Akiweka elfu 10 anapata faida elfu 20, means akiweka na supu, juice, soda, maji, vitafunio, chips anaweza kuingiza hata 60,000 hadi laki kwa siku faida tu.

Huo ni mgawaha mdogo tu wa kawaida na si mikubwa kama ya kina Shishi.

Wafanyakazi wanalipwa hela ndogo tu kama elfu 5 kwa siku... Migawaha ya kawaida hii ina wafanyakazi watatu.... means anatoa elfu 15 anabaki na 45 hadi 85 faida.
 
Kuna wanaolipa kwa sahani anazouza.. Hiyo migahawa ya namna hiyo nguvu kubwa inatumika kusambaza mfano kwanye magerereji, maduka etc. Kwenye center za biashara watu wengi wanapenda kulia kwenye vituo vyao, mfano mtu hawezi kuacha duka akale chakula etc.

Kwa wadada ujira huwa mdogo sana, wapo wanaolipa 3k na ni mjini hapo unajiuliza nauli mtu analipaje na abaki na chochote. Wengi huwa wanadanga unofficially, mchana wanasambaza chakula wakiwa na nguo za jikoni jikoni, jioni wanapita kudai madeni wakiwa na nguo nzuri, wananukia na makeup. Ukijichanganya ndio umemalizia gap lake la mapato.
 
Viti 40 wafanyakazi kama 30. Sidhani kama inawezekana, 30 ni mkusanyiko mkubwa sana asee.
KenMar-Studio-Appleton-Family-Value-Woytych-Fam-9257.jpg
 
Katika biashara ya migahawa mingi huwa naona rundo la wafanyakazi ukilinganisha na ukubwa wa mgahawa.

Kuna mgahawa nimeona una viti 40 na wafanyakazi kama 30 hivi, kuna migahawa midogo midogo ya mtaani mingi ambayo haiwezi hata kukaa zaidi ya watu 5 lakini wafanyakazi wako 5!

Ninachojiuliza mmiliki huwa anagawanyaje mapato kumpatia kila mfanyakazi ujira wake na yeye abakie na faida ya maana pamoja na mtaji wa kuendeleza biashara!
kwani hujui ni kama kwenye ma bar tu kuna wenye ajira zao rasmi na wale wa kula kuona, ama wenye wateja wao wenyewe kimsingi kwenye hizo kazi ukahaba ndio unawaweka mjini same like kwenye salon unakuta mademu wengi kuliko vinyozi yaani ni sheedaaarrrrrr.
 
Katika biashara ya migahawa mingi huwa naona rundo la wafanyakazi ukilinganisha na ukubwa wa mgahawa.

Kuna mgahawa nimeona una viti 40 na wafanyakazi kama 30 hivi, kuna migahawa midogo midogo ya mtaani mingi ambayo haiwezi hata kukaa zaidi ya watu 5 lakini wafanyakazi wako 5!

Ninachojiuliza mmiliki huwa anagawanyaje mapato kumpatia kila mfanyakazi ujira wake na yeye abakie na faida ya maana pamoja na mtaji wa kuendeleza biashara!
Migahawa mingi mjini inategemea usambazaji wa chakula kuliko wanaokuja kula hapo mgahawani. Vilevile wanaweza kuwa wanasambaza maeneo ya mbali kidogo na mengi. Hivyo nguvukazi ni muhimu. Malipo yao ni kidogo japo sio sawa na kuishi bila kazi
 
Back
Top Bottom