Wafanyabiashara wa Nigeria washauriwa kuwekeza Tanzania

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Wafanyabiashara wa Nigeria washauriwa kuwekeza nchini

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Daniel Ole Njoolay, akikata keki huku akishuhudiwa na Mwakilishi wa Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan (wa pili kulia) na baadhi Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Nigeria katika tafrija iliyotayarishwa na Ubalozi wa Tanzania kusherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika hoteli ya Serena jijini Abuja Nigeria mwishoni mwa wiki.



Jumuiya ya wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi wa Nigeria, wameombwa kuja kuwekeza kwa ujumla na kutembelea vivutio vya utalii mbalimbali vinavyopatikana nchini Tanzania.
Wito huo ulitolewa na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Daniel Ole Njoolay, katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yalioandaliwa na ofisi ya ubalozi waTanzania nchini Nigeria na kufanyika katika Hoteli ya Sheraton jijini Abuja.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano hili la Biashara na Uwekezaji, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Daniel Ole Njoolay, alisema Tanzania inajivunia Muungano wake ulioasisiwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na hayati Abeid Amani Karume, Aprili, 1964 ambao sasa umetimia miaka 50.
“Watanzania tunajivunia sana Muungano wetu kwani ni wa kipekee sana hapa barani Afrika, na ni Muungano uliodumu kwa muda mrefu zaidi kuliko muungano wowote ule Barani Afrika”…alisema Balozi Njoolay.
Akizungumzia kuhusu fursa za biashara Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa (Tantrade), Edwin Rutageruka, alisema mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili yameendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na kwamba Tanzania imedhamiria kuendelea kukuza biashara kati yake na Nigeria.
Naye Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo wa EPZ, Lamau Mpolo, alielezea uwapo wa fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo ya gesi na madini.
Alielezea pia namna Serikali ya Tanzania ilivyoweka mazingira mazuri kuvutia wawekezaji kutoka duniani kote katika sekta mbalimbali za uchumi nchini Tanzania.
Akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania vilivyomo katika orodha ya maajabu ya saba\7 ya asili barani Afrika, Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Utalii nchini (TTB), Teddy Mapunda, alisema pamoja na vivutio vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Crater ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi zaidi na vya kipekee.
Alisema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutangaza vivutio vyake saba vya asili ambavyo pamoja na vile vilivyomo katika maajabu Saba ya asili barani Afrika, vivutio vingine ni hifadhi ya taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa ya Kituro, hifadhi ya Taifa ya Gombe na Pori la akiba la Selous. Amewakaribisha wananchi wa Nigeria kutembelea Tanzania na kujionea uzuri na upekee wa vivutio vya Tanzania.
Kongamano hilo lililohudhuriwa na takribani wawekezaji na wafanyabiasha kutoka Nigeria 100, lilifuatiwa na tafrija iliyofanyika usiku katika hoteli hiyo na kuhudhuriwa na waalikwa takribani 350 wakiwamo Mabalozi wa mataifa mbalimbali nchini Nigeria, wageni kadhaa mashuhuri na baadhi ya Watanzania waishio nchini hapa.


CHANZO: NIPASHE
 
duh ole njolay yupo kmbe.....
 
Tanzania hot cake sikuhizi...impressive..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…