Wafanyabiashara wasitake kutumia uhuru waliopewa vibaya, walipe kodi

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Kamwe kama Taifa tusijaribu kuentartain upuuzi wa kukwepa au kutolipa kodi. Mhe. Rais Samia amelegeza masharti ya ufuatiliaji wa ulipaji kodi kwa kundi hili ili kuondoa manung'uniko yaliyotokea katika awamu ya Magufuli.

Wengi wa wafanyabiashara walilalamikia mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwamba ulikuwa ni wa kibabe sana ...mama Samia akaleta maridhiano na akaenda mbali hadi kusamehe madeni halali ya ukwepaji kodi miaka ya nyuma. Inashangaza kuona wafanyabiashara hawa hawa wanaleta kibesi /ubabe hadi kuendesha migomo.

Wito kwa Serikali: Kodi ni takwa la kisheria kwa kila mtu/kada au sekta na hakuna nchi inayochekea watu wake kulipa kodi halali zilizopitishwa bungeni.

Kodi lazima ikusanywe... hakuna upendo kwenye kukusanya kodi.

Kwa leo niishie hapa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Walipe kodi ili mnunulie ma V8 ya kwenda kuwabebea watoto wa chuo siyo!!
Hawa wajinga hata hawajui tatizo liko wapi. Shida sio kodi, shida kubwa ni matumizi ya hizo kodi. Watu wanakamuliwa kodi ili watawala waishi kifalme, wapande magari ya kifahari, shopping Ulaya, watoto wao wako international school kodi milion 40 kwa mwezi, matibabu nje ya nchi.

Wakati huo huo sisi wananchi hatufaidiki na rasilimali zozote zilizopo nchini mwetu. Tuna almasi, tuna dhahabu, tuna uranium, tuna tanzanite tuna gesi, tuna bandari tuna mlima kilimanjaro, tuna mbuga za wanyama, tuna ardhi yenye rutuba, tuna misitu ya asili, tuna vyanzo vya maji safi, lakini serekali inategemea tozo za simu ili ijenge shule. Ifike mahali muone aibu.
 
Hawa wajinga ata hawajui tatizo liko wapi. Shida sio kodi, shida kubwa ni matumizi ya hizo kodi. Watu wanakamuliwa kodi ili watawala waishi kifalme, wapande magari ya kifahari...
Naunga hoja Mkuu! Isitoshe hili suala la Kodi limekaa kinyonyaji sana, unakuta huyu Mfanyabiashara amekopa pesa Bank, analipa huo mkopo kwa riba, analipa Kodi ya Chumba cha Biashara na mambo mengine mengi lakini bado Serikali inataka Kodi kwa huyu Mfanyabiashara ambayo matumizi yake mabovu kama ulivyoeleza hapo.

Wakati huo Nchi Ina rasilimali za kutosha kama ulivyoeleza hapo ambapo kama zingesimamiwa vizuri kusingekuwa na haja ya kuwabana Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla kwa huu unyonyaji wenye jina la Kodi..
 
Kamwe kama Taifa tusijaribu kuentartain upuuzi wa kukwepa au kutolipa kodi.
Mhe.Rais Samia amelegeza masharti ya ufuatiliaji wa ulipaji kodi kwa kundi hili ili kuondoa manung'uniko yaliyotokea katika awamu ya Magufuli...
Wewe hujawahi hata kuuza mapera, unajua nini kuhusu biashara?

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Naunga hoja Mkuu! Isitoshe hili suala la Kodi limekaa kinyonyaji sana, unakuta huyu Mfanyabiashara amekopa pesa Bank, analipa huo mkopo kwa riba, analipa Kodi ya Chumba cha Biashara na mambo mengine mengi lakini bado Serikali inataka Kodi kwa huyu Mfanyabiashara ambayo matumizi yake mabovu kama ulivyoeleza hapo.

Wakati huo Nchi Ina rasilimali za kutosha kama ulivyoeleza hapo ambapo kama zingesimamiwa vizuri kusingekuwa na haja ya kuwabana Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla kwa huu unyonyaji wenye jina la Kodi..
Ni sahihi kabisa.
 
Wanalipa Kodi ndio maana unaona mipango mingi inaenda ukikaa zako bandani huwezi kuona...
 
Kamwe kama Taifa tusijaribu kuentartain upuuzi wa kukwepa au kutolipa kodi. Mhe. Rais Samia amelegeza masharti ya ufuatiliaji wa ulipaji kodi kwa kundi hili ili kuondoa manung'uniko yaliyotokea katika awamu ya Magufuli.

Wengi wa wafanyabiashara walilalamikia mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwamba ulikuwa ni wa kibabe sana ...mama Samia akaleta maridhiano na akaenda mbali hadi kusamehe madeni halali ya ukwepaji kodi miaka ya nyuma. Inashangaza kuona wafanyabiashara hawa hawa wanaleta kibesi /ubabe hadi kuendesha migomo.

Wito kwa Serikali: Kodi ni takwa la kisheria kwa kila mtu/kada au sekta na hakuna nchi inayochekea watu wake kulipa kodi halali zilizopitishwa bungeni.

Kodi lazima ikusanywe... hakuna upendo kwenye kukusanya kodi.

Kwa leo niishie hapa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Mama hataki kodi za zuruma,nawashauri wasilpe tu,tutakopa nje kwa mabeberu kufidia gap
 
Kamwe kama Taifa tusijaribu kuentartain upuuzi wa kukwepa au kutolipa kodi. Mhe. Rais Samia amelegeza masharti ya ufuatiliaji wa ulipaji kodi kwa kundi hili ili kuondoa manung'uniko yaliyotokea katika awamu ya Magufuli.

Wengi wa wafanyabiashara walilalamikia mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwamba ulikuwa ni wa kibabe sana ...mama Samia akaleta maridhiano na akaenda mbali hadi kusamehe madeni halali ya ukwepaji kodi miaka ya nyuma. Inashangaza kuona wafanyabiashara hawa hawa wanaleta kibesi /ubabe hadi kuendesha migomo.

Wito kwa Serikali: Kodi ni takwa la kisheria kwa kila mtu/kada au sekta na hakuna nchi inayochekea watu wake kulipa kodi halali zilizopitishwa bungeni.

Kodi lazima ikusanywe... hakuna upendo kwenye kukusanya kodi.

Kwa leo niishie hapa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
What do you do for a living champ
 
Pumbav kabisa, watumishi wa Umma mna shida sana. kutwa hamwishi kulalamika munataka nyoongeza.
 
Tuoneshe TIN na VRN zako ndo tuanze kuongea sio unaleta polojo za kishamba
 
Back
Top Bottom