Wafanyabiashara wote wanapenda kukwepa kulipa Kodi

Wafanyabiashara wote wanapenda kukwepa kulipa Kodi

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Hakuna mfanyabiashara yeyote Duniani na haswa kwa Nchi za Afrika anayependa kulipa Kodi, wengi wao huwa wanatafuta mianya ya kukwepa kulipa Kodi.

Wafanyabiashara wengi wanatafuta faida zaidi kwa njia yoyote ile.

Hivyo kujadiliana kuwa Kodi hii ilipwe ama isilipwe ni sawa na nyani kulinda shamba la mahindi!

Jambo la msingi Serikali iweke utaratibu mzuri wa kulipa Kodi na sio Kodi kufutwa, hakuna nchi inayo weza kuendeshwa bila Kodi.

Ku negotiate namna ya kulipa Kodi ni sawa na kutaka kuhujumu uchumi wa nchi.

Kodi ni ya wananchi wenyewe sio ya Serikali.

Ukiruhusu kujadili Kodi flani isilipwe nyingine ilipwe ni jambo la hatari sana......lenye nia na lengo la kuhujumu uchumi wa nchi.

Serikali Ina onyesha uungwana lakini wafanyabiashara sio waungwana. Wanacho taka wao ni Kukwepa Kodi.
 
61qpWAn6sQL._SY445_.jpg
 
Hakuna mfanyabiashara anayependa kukwepa kodi. Misingi ya sheria zetu zinashawishi watu tukwepe kodi.

Huwezi niambia nilipe 0.03 ya mauzo yangu kama service levy. Unakutana mtaji wa million 20. Nikizungusha mara 5 kwa mwezi ni million 100.

Huwezi weka million 100 kigezo cha vat kwa mtu anayeuza bidhaa moja mfano gari moja tuu million 35
 
Kodi italipwa na itaendelea kulipwa ila wafanyabiashara ni sahihi kusikilizwa.
Wasikilezwe lkn wasitake kusamehewa Kodi.

Kodi ya Nchi lazima ilipwe hakuna msamaha kwenye Kodi.

Ila utaratibu uwe imara na sahihi sio vurugu.

Kodi ilipwe Hilo halina namna
 
Wasikilezwe lkn wasitake kusamehewa Kodi.

Kodi ya Nchi lazima ilipwe hakuna msamaha kwenye Kodi.

Ila utaratibu uwe imara na sahihi sio vurugu.
Hakuna nchi inaenda bila kodi. Wafanyabiashara wanategemewa katika kodi, tunawategemea sana tusikilizane.
 
As long as nchi inaenda kifisadi fisadi, hakuna mfanyabiashara aliyepo tayari kulipia mafuta ya mashang'ing'i ya mafisadi, huu ni mwanzo tu.

Hili suala ni indicator ya jambo kuu lijalo
 
  • Thanks
Reactions: apk
As long as nchi inaenda kifisadi fisadi, hakuna mfanyabiashara aliyepo tayari kulipia mafuta ya mashang'ing'i ya mafisadi, huu ni mwanzo tu.

Hili suala ni indicator ya jambo kuu lijalo
Maduka yote kkoo yamefunguliwa na watu wanapiga mishemishe.

Biashara lazima zifanyike na Kodi ya Serikali lazima ilipwe Hilo sio hiari.

Hakuna nchi yoyote Duniani inayo endeahwa bila Kodi ila watanzania ndio wanataka wafanye biashara bila kulipa Kodi!!! Maajabu haya!!!

Kama unataka kufanya biashara basi jua Kodi ni lazima kama hutaki nenda ukafanye kazi zingine.
 
Ndio maana awamu ya 5 chini ya Hayati JPM hakutaka mchezo kwenye kukusanya Kodi.
Kodi ilikusanywa kwelikweli
Acha mahaba, Kodi siku zote zinaongezeka huyo unayemtaja alitakewa aweke vizuri mifumo!! Ila Kwa Sasa hawezi kutusaidia tena
 
Kama inakataa, hafu kama inakuja vile..
 
Hakuna mfanyabiashara yeyote Duniani na haswa kwa Nchi za Afrika anayependa kulipa Kodi, wengi wao huwa wanatafuta mianya ya kukwepa kulipa Kodi.

Wafanyabiashara wengi wanatafuta faida zaidi kwa njia yoyote ile.

Hivyo kujadiliana kuwa Kodi hii ilipwe ama isilipwe ni sawa na nyani kulinda shamba la mahindi!

Jambo la msingi Serikali iweke utaratibu mzuri wa kulipa Kodi na sio Kodi kufutwa, hakuna nchi inayo weza kuendeshwa bila Kodi.

Ku negotiate namna ya kulipa Kodi ni sawa na kutaka kuhujumu uchumi wa nchi.

Kodi ni ya wananchi wenyewe sio ya Serikali.

Ukiruhusu kujadili Kodi flani isilipwe nyingine ilipwe ni jambo la hatari sana......lenye nia na lengo la kuhujumu uchumi wa nchi.

Serikali Ina onyesha uungwana lakini wafanyabiashara sio waungwana. Wanacho taka wao ni Kukwepa Kodi.
Mawazo haya ndiyo yaliyoko kwa Vijana wengi walioajiriwa na TRA.

Hakuna Mfanyabiashara anayetaka kukwepa Kodi wakati Biashara ndiyo Maisha yake!

KODI NI SEHEMU YA BIASHARA.

Lakini BIASHARA NI KAMA MTOTO ALIYEZALIWA.

Mtoto akilelewa Vibaya mwishoni atakuwa CHOKORAA.

Mazingira ya Biashara yenye usawa na yaliyoandaliwa Vizuri na Mifumo ya Serikali yanamsaidia Mfanyabiashara kulipa Kodi Vizuri sana!

Vijana wadogo wa TRA wamesoma Sheria za Kodi na kuzitafsiri wakati mwingine kwenye mazingira yasiyofaa.

Hawamsikilizi Mlipa Kodi kwa maana ya Kushiriki kuelewa Mazingira yake ya Biashara!

Mfano:
Mfanyabiashara wa Samaki anahitaji UMEME WAKATI WOTE ILI AWEZE KUFANYA BIASHARA YAKE VIZURI...

Umeme unapokatika na tena bila Taarifa tayari umekwishamsababishia matatizo makubwa kwenye Biashara yake!

Kipindi cha Shida kama hizo zikimpata Mfanyabiashara hakuna sekta hata moja itakayokuwa tyr kumsikiliza na kumsaidia ...iwe ni Bank au ni Tra...hapa wanafuata Sheria za Kikodi...wanaishia kuua Biashara...

Kila mtu anaona Jitihada za Serikali kwenye kujenga uchumi mkubwa.

Hizi ni Jitihada kubwa na za kututia Moyo sisi wafanyabiashara...

Awamu hii wafanyabiashara tunapanga KUFANYA Biashara na kukua kwa Sababu Dhamira ya Mh Rais tunaiona...

Na kodi pia inaongezeka na sisi tunafurahi kisikia makusanyo yanapanda...LAKINI TUNAHITAJI KUSIKILIZWA NA WATOZA USHURU.

WATOZA USHURU WAJITAHIDI KUJIFUNZA NA KUELEWA BIASHARA NA KUZISAIDIA KUKUA.

Kulipa Kodi ni Fahari lakini siyo kulipa mitaji kama kodi...!
 
Acha mahaba, Kodi siku zote zinaongezeka huyo unayemtaja alitakewa aweke vizuri mifumo!! Ila Kwa Sasa hawezi kutusaidia tena
Kodi lazima ilipwe ila mifumo iwekewe utaratibu unao eleweka. Lkn kama unadaiwa Kodi halali hakuna jinsi zaidi ya kulipa.

Kuna mama mmoja mfanyabiashara eti anadai kwa waziri Mkuu alipe Kodi anayo itaka yeye!!!!

Haiwezekani, lazima Kodi ilipwe
 
Maduka yote kkoo yamefunguliwa na watu wanapiga mishemishe.

Biashara lazima zifanyike na Kodi ya Serikali lazima ilipwe Hilo sio hiari.

Hakuna nchi yoyote Duniani inayo endeahwa bila Kodi ila watanzania ndio wanataka wafanye biashara bila kulipa Kodi!!! Maajabu haya!!!

Kama unataka kufanya biashara basi jua Kodi ni lazima kama hutaki nenda ukafanye kazi zingine.
Acha upngo kwa kusema maduka yote yanefunguliwa nenda kule kwenye nguo uone kana wamefungua
 
Back
Top Bottom