Wafanyakazi IPTL waendelea kuililia Serikali

Wafanyakazi IPTL waendelea kuililia Serikali

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) wameendelea kuiomba serikali iwasaidie kulipwa stahiki zao wanazoidai kampuni hiyo.Wafanyakazi hao walioachishwa kazi 31 october,2018 wamekuwa wakifuatilia stahiki zao bila mafanikio.

Wafanyakazi hawa wanaiomba serikali kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu aweze kuwasaidia kulipwa haki na stahiki zao kwani wanaishi maisha magumu na wanaumia kwani walifanya kazi kwa uadilifu na kwa muda mrefu lakini katika swala la kupewa stahiki zao limekuwa gumu.

”Tunaamini kwa kuwa ofisi yako ndio inashughulikia madeni yote ya IPTL ikiwemo la Standard Chartered na stahiki zetu zitashughulikiwa,” wamesema wafanyakazi hao.

IMG-20230703-WA0009.jpg
IMG-20230703-WA0008.jpg
IMG-20230703-WA0010.jpg
IMG-20230703-WA0011.jpg
 
Back
Top Bottom