Wafanyakazi: Kuna kazi aina nyingi duniani na zote zinategemeana

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Nyingine zinahitaji ujuzi, elimu na tajriba ya kiwango cha juu ukilinganisha na nyingine.
Mifano​
1. Mhasibu: Mtaalamu wa kuweka hesabu ya fedha.

2. Mhandisi/injinia: Mjuzi wa kutengeneza, kuhudumia na kuunda mitambo.

3. Tarishi/Katikiro: Anayehudumu ofisini kwa kutumwa kupeleka habari au ujumbe.

4. Bawabu: Alindaye mlangoni.

5. Topasi/chura: Asafishaye choo.


6. Tabibu/daktari/mganga: Mwenye ujuzi wa kutibu.

7. Muuguzi/mualisaji: Ahudumiaye wawele/wagonjwa

8. Msarifu: Anayesimamia na kuidhinisha matumizi mazuri ya fedha katika shirika.
9. Dereva: Aendeshaye vyombo vya nchi kavu k.v. gari

10. Nahodha: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya majini k.v. meli



11. Rubani: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya angani k.v.ndege

12. Utingo/taniboi: Mpakiaji na mpakuaji wa mizigo katika gari.

13. Hamali/mpagazi/mchukuzi: Abebaye mizigo kwa malipo.

14. Machinga: Auzaye bidhaa rejareja kwa kuzungukazunguka.

15. Malenga: Mtunzi stadi wa mashairi na nyimbo.

16. Manju: Stadi wa kutunga na kuimba nyimbo katika ngoma.

17. Kuli: Apakiaye na kupakua shehena za forodhani.

18. Dobi: Afuaye na kupiga nguo za watu pasi kwa malipo.
 
19. Sogora: Fundi wa kupiga ngoma.

20. Saisi: Atunzaye wanyama wanaopandwa k.v. punda na farasi.



21. Msajili: Awekaye orodha ya kazi, vitu au viumbe.
View attachment 823781
22. Mkalimani/mtarijumani: Afasiriaye lugha moja hadi nyingine.

23. Sonara: Atengenezaye mapambo kwa kutumia madini.

24. Kinyozi: Anyoaye nywele.

25. Msusi/msosi: Asukaye watu nywele.

26. Ngariba: Apashaye wavulana tohara katika jando.

27. Mkunga: Awasaidiaye wajawazito kujifungua.

28. Kungwi: Afundishaye mwari wa kike au kiume.
29. Mhariri: Asomaye, kusahihisha na kusarifu makala, magazeti n.k.

30. Mshenga: Atumwaye kupeleka habari za ndoa (posa).



31. Refa: Mwamuzi katika mchezo k.v. soka.

32. Kasisi: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kikristo.

33. Imamu: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kiislamu.

34. Hakimu: Aamuaye kesi katika mahakama.

35. Kadhi: Hakimu wa kiislamu.

36. Mlariba: Akopeshaye wengine pesa.

37. Mwekezaji: Anayeweka mali au pesa katika mradi au biashara.

38. Meneja: Msimamizi au kiongozi katika kampuni au shirika.
 
39. Karani: Afanyaye kazi ya kuandika k.m. barua na majarida.

40. Kocha: Mwalimu wa mchezo k.v. soka.



41. Mkutubi: Ahifadhiye vitabu maktabani na kuviazimisha.

42. Mnajimu: Mwenye elimu ya nyota. Hutabiri mambo.

43. Mpigaramli: Abashiriaye kwa kupiga bao.
44. Mwajiri: Aandikaye mtu kwa kazi ya malipo au mshahara.

45. Mzegazega: Achotaye maji na kuyauza.

46. Dalali: Auzaye bidhaa katika mnada (soko la kushindania bei)

47. Manamba: Mfanyikazi wa muda katika shamba kubwa.
[resource: 2977, align: left]
48. Mnyapara: Msimamizi wa kazi.

49. Mhazili: Sekretari - Atunzaye barua na majarida na kuandika kwa mashine ofisini.

50. Mhadhiri: Mwalimu katika chuo kikuu.



51. Mwashi: Ajengaye nyumba kwa mawe.

52. Mhunzi: Afuaye vitu vya madini ya chuma au bati.

53. Seremala : Atengenezaye samani za mbao au miti.

54. Mfinyanzi: Atengenezaye vyombo vya udongo k.m. vyungu.

55. Mvuvi: Afanyaye kazi ya kuvua samaki.

56. Mwanaanga: Afanyaye utafiti wa hali ya anga.

57. Mkabidhi: Mtu atunzaye mali kwa ajili ya mwengine
58. Diwani: Anayewakilisha watu wake katika serikali za wilaya
59. Mzoataka: Anayeokota takataka

60. Kaimu: Anayeshikilia cheo au wadhifa fulani kwa muda


Zoezi A.
Zitaje kazi za wafuatao.
  • Mwalishi
  • Sarahangi
  • Mchuuzi
  • Mwamizi
  • Mfugaji
  • Mamantilie
  • Mlumbaji
  • Mgema
  • Mbunge
  • Baharia
  • Wakili
  • Mjumu
  • Diwani
  • Mrumba
  • Kandawala
  • Gambera


B. Taja watu wazifanyazo kazi hizi.
Aliyesomea diplomasia ni_________
Mtu afanyaye utafiti wa mambo ya sayari za juu__________
Mchezaji wa mpira wa miguu ni __________
Afanyaye kazi katika meli ni __________ .
Achezaye michezo ya riadha ni __________.
Raia anayejitolea kufanya kazi ya ulinzi ni __________
Askari katika jeshi la ulinzi __________
Anayeshughulika na sheria ni __________.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…