Wafanyakazi nchini Kenya kuanza kukatwa mishahara kusaidia ujenzi wa nyumba

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
KUANZIA mwezi huu, wafanyakazi wa nchini Kenya wataanza kukumbana na maumivu ya makato katika mishahara yao kwa kiasi cha asilimia 1.5 kwa ajili ya kodi ya nyumba.

Makato hayo yataelekezwa katika mpango wa serikali wa kujenga nyumba za bei nafuu nchi nzima. Nyumba 2,000 za kwanza zitajengwa Nairobi hivi karibuni.

Wizara ya Usafirishaji, Miundombinu, Nyumba, Maendeleo ya Makazi na Kazi za Umma kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA), wamethibitisha kukamilika kwa mpango wa kuanza makato hayo.

“Mwajiri na mwajiriwa wote lazima wachangie asilimia 1.5 ya mshahara wa mfanyakazi wa mwezi ili mradi tu kuwa michango jumla ya mfanyakazi haiwezi kuzidi shilingi za Kenya 5,000,” alisema mmoja ya wataalamu wa fedha nchini Kenya.

Wizara hiyo ilisema fedha zitakazokusanywa katika mpango huo, zitatumika katika kujenga nyumba za bei nafuu kwa ajili ya wananchi wa hali ya chini. Hii ni moja ya ajenda za chama tawala nchini Kenya cha Jubilee katika ajenda zake nne za kuwatumikia wananchi.

Serikali ya Kenya ya Rais Uhuru Kenyatta ilipanga kuanza makato hayo kuanzia Januari mwaka huu, lakini Chama cha Wafanyabiashara na Wafanyakazi (COTU) kilikwenda mahakamani kupinga makato hayo.

Waziri wa Usafirishaji, Nyumba na Miundombinu, James Macharia aliwaambia wanahabari kuwa ujenzi wa nyumba hizo, utaanza baada ya makato ya asilimia 1.5 kwa wafanyakazi wote kuanza na shughuli hiyo itaanza katika wiki chache zijazo.
 
Duh, hii si ndio extreme socialism, in a capitalistic country chini ya uongozi wa manyang'au.
All de best mazee, poleni sana wafanyakazi.
 
Angalau KIBETA. MATHARE and the likes watapata ahueni. Povu ruksa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Halafu wanaenda kujenga nyumba kwenye ardhi ya kenyata family.
 
Wakenya Ahaaa haaa haaa.
Yaani mnaanza kukatwa mshahara bila sheria wala nini. Sasa aggressiveness yenu iko wapi?
 
WAZO ZURI NDUGU ZETU EMBU ENDELEENI KUJENGA INCHI MAANA INCHI INAJENGWA NA WANANCHI NA SIO WAHISANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…