Wafanyakazi PSSSF HQ wanashiriki kutapeli wastaafu

Wafanyakazi PSSSF HQ wanashiriki kutapeli wastaafu

NDAGLA

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2012
Posts
2,490
Reaction score
1,353
Kwema wadau,

Natoa tahadhari kwa wote wanaowasiliana na PSSSF kupitia DM page yao rasmi ya instagram (Psssftz) na wale wanaopiga namba zao za bure 0800110040 na 0800110055 kuhitaji msaada wowote.

Kwa kifupi watumishi wa kitengo hicho cha huduma kwa wateja ukishawasiliana nao watakuomba namba yako ya uanachama then watakupigia wao kwa namba zao binafsi (siyo za ofisi) na ndipo watakupa taarifa za kupotosha na wanatumia njia hii kutapeli watu fedha.

Wakifanikiwa kutapeli,hutojibiwa email,DM instagram tofauti na awali na ukipiga hizo simu za ofisi hutopata ushirikiano zaidi watakata na kukupigia kwa namba zao binafsi na kujibu kejeli.

(Ni kama watu wengi wanashirikishana huu utapeli)

Mbaya zaidi huu utapeli unasemwa ni agizo kutoka kwa Rais kwamba wastaafu walipie hizo control number.

Inawezekanaje taasis kama PSSSF isiweze kuwa na taarifa za nani alimhudumia mteja siku na saa fulani kupitia page yao ya instagram?

Hata records za siku tatu nyuma!

You're warned.
 
Mbona hujaweka wazi huo utapeli unakuaje... Ni kwamba wanakomba michango yako au?




Cc: mahondaw
Wala hawachukui michango!

Wanaotapeliwa ni wastaafu ambao Mwajiri wao hakuwasilisha michango yao yote PSSSF.

Wanaambiwa walipe (wastaafu) wenyewe hiyo michango ambayo (haikuwasilishwa) directly PSSSF ili walipwe pension iliyobaki kwa madai ni agizo la Rais.

Hao wafanyakazi wanatoa namba za akaunti binafsi ama watumiwe kwa njia ya simu ili wawasaidie kulipia kinachoitwa Cheque control number zao.

Hope nimeeleweka.
 
Shida ni kwamba,huu utapeli unafanywa na wafanyakazi wenyewe siyo outsiders maana mawasiliano yanaanzia kwenye mfumo wao rasmi wa huduma kwa wateja ndio wanahamia uchochoroni.
 
Kuna haja ya Psssf kuweka mfumo ambao itakuwa rahisi wao kumfahamu mfanyakazi wao aliyetoa huduma kwa mteja kuoitia mitandao yao muda na siku husika.
 
Wastaafu nao dah vingine vinonko na vinaa kazini utadhani wanafia kazini dah ila maisha haya ni kama mbio za vijiti
 
Hata sasa hivi wastaafu wakidai pesa zao wanaambiwa wanasubiri rais asaini ndipo wapewe pesa zao.

Miujiza mitupu
 
Back
Top Bottom