Wafanyakazi tunaumia kwa mzigi wa kodi

Wafanyakazi tunaumia kwa mzigi wa kodi

kamkoda

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
396
Reaction score
71
Mimi nashauri TRA isimamiwe na taasisi huru ili kukagua maeneo ya kodi ambazo hazijalipwa. Hapa mjini kuna maduka ya hardware hayaguswi hata kidogo kwa kuwa wenye mali wanautaratibu na maofisa waandamizi wa TRA. Kuna ofisa mmoja pale USA RIVER ( wa TRA yeye anazungukia makampuni ya kitalii na kuwatengenezea hesabu ili mambo yao yawe mazuri) huyu nahisi anatakiwa kushughulikiwa na vijana wa uamsho.

Nina hasira sana jasho langu linarambwa muno!
 
Mkuu wangu,
unadhani yuko peke yake ? Huo ni mtandao wa wachakachuji wanaojali matumbo yao na ya marafiki zao tu. Wezi wakubwa, wasio na huruma.
Narudia kusema hao ni wajumbe wa ibilisi yule shetani mtembea kwa miguu. Wanaibia nchi kwa kudhamiria siku zote ili watajirike, duh !!
Iwepo sheria ya wananchi wenye hasira kali waliojua maovu yao wawatwange na kuharibu historia yao mbaya, na wasihukumiwe kwa maana wanadai haki yao ya msingi toka kwa wezi wachache.
 
Mie nakubaliana nawe. kodi za wafanyakazi ndo zinaendesha sirikale ya mk.w.re. tra imefunga ndoa na wezi na wahujumu, huku wafanyakazi hawana pa kutokea. tra inawaogopa wanyabiashara. ngoja niache kazi nikafanye biashara sasa.
 
Back
Top Bottom