Wafanyakazi wa Bomba la Mafuta (ECOP) Mkoa wa Singida walalamikia mafao yao kutopelekwa NSSF, pamoja na kodi TRA

Wafanyakazi wa Bomba la Mafuta (ECOP) Mkoa wa Singida walalamikia mafao yao kutopelekwa NSSF, pamoja na kodi TRA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wafanyakazi wa wanaojihusisha na ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Mkoani Singida wamedai haki zao katika Mifuko ya Jamii (NSSF) pamoja na kodi wanayokatwa ifike katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo kwa sasa haifiki kwa wakati kutoka katika Kampuni ya Nantong Construction Group (T) LTD wanayo ifanyia kazi.

Wafanyakazi 27 kutoka katika Kampuni ya Nantong Construction Group (T) LTD wamefika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Singida kuomba msaada ili changamoto zao ziweze kutatuliwa.

Wamedai nyaraka za mshahara zinaonesha makato ya kodi pamoja na NSSF lakini walipofuatilia hakuna pesa zilizoingizwa katika Mamlaka ya mapato au NSSF.

Aidha, Wafanyakazi hao wameelekeza kero zao katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Singida ili kupewa msaada.

Wafanyakazi hao wamepokelewa na Afisa Tawala Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, Omary Ramadhani Kasele ambapo baada ya kuwasikiliza amewaita maafisa wa TRA na NSSF il ikupata maelezo kutoka kwao.

Upande wake Meneja Msaidizi wa TRA - Singida, Sadru Adam Kamugisha amedai kuichukua kero hiyo na kuahidi kufuatilia katika kampuni yao na kujua namna gani wanawajibika katika ulipaji wa kodi kama ambavyo taarifa ilivyo.

Naye, Afisa Mafao Mwandamizi wa NSSF Singida, Mzee Shabani Mwinyi ametoa elimu namna wanavyotakiwa walipiwe mafao kila mwezi pamoja na kuwaomba Wafanyakazi hao wafike ofisini ili wakawasikilize zaidi na kuwapatia msaada.

Pia soma ~ Wabunge Waalikwa Kutembelea Mradi wa ECOP
 
Back
Top Bottom