Archnemesis 2-0
JF-Expert Member
- Aug 25, 2024
- 815
- 1,558
Kwema Wadau,
Kama mnakumbuka mwezi wa 8 hapa katikati wafanyakazi wa Jomo Kenyatta International Airport walifanya mgomo.. kwa kweli niliona ile ishu juu juu skufatilia zaidi.
Sasa hapa nasikiliza D.W lunch time nasikia shughuli zote za usafiri JKIA zimesimamishwa na wafanyakazi wamegoma mgomo wa amani wakitaka majibu kutoka kwa uongozi.
Wanataka waelekezwe mkataba mpya wa muwekezaji wa India kampuni ADANI iliyopewa miaka 30 ya kuendesha shughuli za airport. Wafanyakazi wa airport za Mombasa na Eldoret wamegoma pia..
Ila hawa jamaa wana misimamo!
Attached is the Voice Record.. sehemu ya taarifa.