Hivi supose ukienda masomon mf. Kwa miaka 3,bahati mbaya ukakumbwa na CARY AU RETAKE yaani unatakiwa kuongeza mwaka 1 zaidi ili uhitimu. Utaombaje ruhusa tena kwa mwajiri wako? Ili uweze kumalizia mwaka mmoja uliobaki ktk masomo yako!
Ayse pole kwa maelezo yako ni dhahiri kwamba umefeli na unataka kujua namna ya kuandika hiyo barua ueleweke. Sasa nakushauri kama nchini nenda zungumza ana kwa ana na mkurugenzi au CEO wa hiyo taasisi ueleze ukweli kwamba mzee mambo siyo nimevuruga akusaidie mwaka mmoja ujitahidi umalizie maana ukiacha hapo miaka mitatu iliyopita ni sawa na bure. Kufanya hivyo ni muhimu maana utaonekana umetoroka na utakiuka makubaliano na utafutwa kazi. Pia unaweza kuhisiwa kuwa unaendelea na masomo ya juu zaidi uje uchukue nafasi ya bosi kumbe maskini ya Mungu umefeli. Ila jitahidi bwana usome kwa bidii acha starehe wakati wa masomo umalize urudi job si unajua nchi yetu maskini nenda kafanye kazi!