A
Anonymous
Guest
Sisi wafanyakazi wa SGR kwa sasa tupo nyumbani tukiwa hatujui hatima yetu juu ya kinachoendelea kuhusu project hiyo hasa kuanzia Lot 3 na 4.
Ipo hivi, Lot 3 na 4 kwa sasa zimesimama, wafanyakazi tuliokuwa katika mradi huo kwa sasa tupo tu nyumbani, awali tuliambiwa tukae nyumbani hadi tutakapojulishwa, wengine wakaambiwa wakae home kwa wiki mbili.
Zilipoisha, tukarejea kazini, tukakutana na agizo lingine kuwa tunatakiwa kuendelea kuwa nyumbani kwa wiki mbili nyingine.
Upande wa wenzetu ambao wapo Lot 5 (Isaka - Mwaka) na 6 (Tabora - Kigoma) napo hali ni hivyohivyo kwa kuwa huko walikuwa katika mchakato wa kuanza, mambo yamesimama na hakuna kinachoendelea.
Pamoja na yote jambo la kushukuru ni kuwa tunaendelea kulipwa kama kawaida, japo tunalipwa basic salary bila nyongeza nyingine yoyote, wale ambao hawakuwa na mkataba wao hawalipwi.
Jambo la kusikitisha ni kuwa pamoja na yote hayo yanayoendelea maingizo ya fedha zetu za NSSF hayajaingizwa tangu Desemba 2022 licha ya kuwa watu tumekuwa tukikatwa kwenye mishahara yetu kwa muda wote huo.
Pia soma ~ Serikali yashindwa kulipa wakandarasi, mradi wa SGR Mwanza wasimama