BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
na Edson Kamukara | Tanzania Daima | Oktoba 09, 2012
SIKU chache baada ya Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, kuahidi kuwavalia njuga baadhi ya wafanyakazi wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha utaratibu na kufanya kazi bila vibali, msako mkali umeanza kwenye baadhi ya mahoteli jijini Dar es Salaam.
Dk. Mahanga alitoa ahadi hiyo baada ya gazeti hili kuripoti taarifa za kushamiri kwa wageni hao kwenye makampuni kadhaa ya kigeni na mahoteli makubwa jijini Dar es Salaam na kuajiriwa kufanya kazi za kawaida ambazo kwa mujibu wa sheria za nchi zinapaswa kufanywa na raia wa Tanzania.
Katika mfululizo huo wa habari hizo, ilitajwa pia moja ya hoteli kubwa iliyoko eneo la Kunduchi pamoja na kampuni moja ya Kichina iliyoko eneo la Ubungo, ambapo wameajiriwa raia wengi wenye asili ya India na China ambao baadhi yao hawana vibali vya kazi wala ujuzi wa kazi walizoajiriwa kufanya.
Hata hivyo, hatua hiyo ilielezwa kuwa inachangiwa na baadhi ya watendaji wa wizara za Mambo ya Ndani kupitia Idara ya Uhamiaji na ile ya Kazi na Ajira ambazo hutoa vibali hivyo.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwepo madai ya baadhi ya watendaji wanaotoa vibali kinyemela kwa wageni hao na hivyo kusababisha raia wa Tanzania wenye sifa kukosa ajira kwenye makampuni na mahoteli husika.
Tuhuma hizo zilithibitishwa pia na mmoja wa viongozi wa juu wa hoteli moja iliyopo Kunduchi ambayo inalalamikiwa, akidai kuwa watendaji wa wizara hizo wameendekeza rushwa na hivyo hata wanapokwenda kuzikagua hoteli hizo, wanachukua kitu kidogo kutoka kwa wamiliki.
"Mimi si msemaji wa hoteli kuhusu jambo hilo unaloliuliza lakini nikwambie kuwa anayeidhinisha sifa za wageni hao kama wana sifa au la ni mwajiri. Pili watu hawa wako nchini kihalali wakiwa wameidhinishwa na serikali.
Kuhusu madai ya uongozi wa hoteli hiyo kutoa rushwa kwa maofisa wa serikali ili kuwalainisha wasiwasumbue wageni hao, alikiri kuwa ni kweli na kutamba: "Kama tunao uwezo huo wa kufanya hivyo kwa nini tusifanye?
Kufuatia madai hayo, Naibu Waziri Mahanga, aliliambia gazeti hili kuwa apewe muda kidogo ili aweze kutuma wasaidizi wake kuzikagua kampuni na hoteli hizo kuona ukweli wa malalamiko hayo, huku akisisitiza kuwa vibali vya kazi kwa wageni ni vya miaka miwili na kwamba hakuna anayeruhusiwa kufanya kazi bila kuwa na kibali husika.
Hata hivyo alikiri kuwepo kwa msigano baina ya wizara hizo mbili akisema kuwa wanaandaa muswada ili jukumu la utoaji vibali hivyo libakie chini ya wizara moja tofauti na sasa ambapo wizara ya kazi inamwidhinisha mgeni na kupeleka taarifa zake Idara ya Uhamiaji kumwombea kibali.
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili limezipata, zinasema kuwa mara mbili katika wiki iliyopita, watendaji wa wizara hizo wamefika katika hoteli hiyo yenye wafanyakazi wa kigeni zaidi ya 29 na kufanya mahojiano na baadhi yao sambamba na kukagua vibali vyao vya kazi.
Chanzo hicho kimebainisha kuwa mchakato huo hata hivyo umeingia dosari kutokana na wafanyakazi hao wengi wao kutimkia kujificha kusiko julikana kila maafiasa wa wizara wapofika hotelini hapo.
"Watendaji wa wizara walifika hapa katikati ya wiki lakini wafanyakazi wengi walikimbilia kujificha na hivyo hawajahojiwa wala vibali vyao havijakaguliwa, zaidi tumeona uongozi wa juu ukijaribu kuwashawishi walimalizane," kilisema chanzo chetu.
Pia kwa mara nyingine siku ya Ijumaa, watendaji hao wa wizara walifika hotelini hapo lakini wafanyakazi wengi wa kigeni wanadaiwa kukimbia wakikwepa kuhojiwa.
Mbali na baadhi kujificha, mameneja watatu wa hoteli hiyo waliangukia mikononi mwa maofisa hao wa uhamiaji.Walionaswa na kuhojiwa ni meneja matunzo,meneja anayesimamia usafi na meneja wa mapishi.
Waliofanikiwa kuwakwepa maafisa hao ni pamoja na mhesabu mashuka na taulo, mkagua bili, msimamizi wa baa, mpishi, fundi na wengine. Taarifa hizo ziliongeza kuwa baada ya ukaguzi, baadhi ya wafanyakazi hao waliokuwa wamekamatwa walibainika kuwa na vibali halali licha vibali hivyo kuwa na mashaka.
"Waliobakia wawili hawakuwa na vibali, hivyo maafisa hao walikwenda nao ofisini kwao lakini baada ya takribani saa tatu walirudi kazini na kuendelea na kazi," chanzo chetu kilisema.
Idadi ya wageni wanaoishi na kufanya kazi nchini imekuwa ikiongezeka kwa kasi kiasi cha kutishia ajira za wazawa kwani kazi nyingi wanaoajiriwa kuzifanya zinaweza kufanywa na Watanzania.
Msemaji wa mmiliki wa hoteli hiyo, alipohojiwa na gazeti hili alishindwa kufafanua ni kwanini raia hao wa India wanaletwa kufanya kazi za kawaida ambazo nyingine hazina utalaamu wowote.
Badala yake, alitetea kuwa huo ni uamuzi wa mwenye hoteli kuajiri wafanyakazi atakavyo na kwamba wengi wao ni raia wa Tanzania wenye asili ya India.
"Hao wanaolalamikiwa si wageni kutoka nje, wengi wao ni Watanzania wenye asili ya India, wanawahukumu kwa rangi zao. Wala hawafanyi kazi hapa hotelini wote, sisi tuna makampuni kama 18, sasa wakiwaona humu wanadhani wameajiriwa," alitetea.
Akizungumza na gazeti hili jana, msemaji wa Idara ya uhamiaji, Abbas Irovya, alikiri kufanyika kwa msako huo akifafanua kuwa huo ni utaratibu wao wa kawaida ili kuwabaini wanokiuka sheria.
Kuhusu baadhi ya wageni kuwapiga chenga, alisema hiyo ni hali ya kawaida kwa kila mwarifu na hivyo akaomba wazalendo kutoa ushirikiano ili wahusika wakamatwe.
Abbas alikiri kusikia tuhuma za rushwa kwenye idara yao lakini akafafanua kuwa jambo la msingi ni wananchi kupewa elimu ya kutosha wakajua vyema majukumu ya idara ya uhamiaji.