kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,015
Ninaomba tafsiri ya wanyonge kwa nchi hii tafadhali?
Maana ninapata shida kusikia Boda Boda ni mnyonge, na nina ushahidi hawa vijana wa Boda Boda, wanaingiza kipato zaidi ya shilingi laki sita kwa mwezi. Mfanyakazi mwenye mshahara wa laki tatu hadi laki tano, mkataba wake unaisha, ananyimwa mafao yake aliyokuwa akikatwa kwenye mshahara. Huyu inaonekana si mnyonge.Ila mama lishe anayeuza mauzo ya siku elfu 50, hakosi faida ya laki 6 kwa mwezi, ni mnyonge!
Dereva amemuendesha mkuu wa mkoa miaka 20 bila ajali, anaondolewa kazini eti ni darasa la saba, bila mafao yoyote, wakati kuna mtu amepewa ukuu wa mkoa, ana cheti feki cha form four!?
Huyu mnyonge wa Tanzania ana sifa gani?
Nielewesheni nijue nini maana ya mnyonge