A
Anonymous
Guest
Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway “SGR” kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza unaendelea ukiwa na jumla ya Kilometa 1,219, bado kuna mambo kadhaa hayaendi sawa.
Licha ya Serikali ya Tanzania kuweka wazi kuwa imekamilisha malipo hadi hatua ilipofikia kwa Mkandarasi reli hiyo (Kampuni ya Yapi Merkezi) bado kuna changamoto ya Wafanyakazi Wazawa kutoingiziwa stahiki zao za malipo ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa miezi 8.
Ipo hivi, sisi Wafanyakazi Wazawa hasa tuliopo katika Lot 1 na 2, tunatarajia kufanya mgomo wa kutofanya kazi katika mradi kuanzia mwezi wa tisa tarehe 6, mwaka huu (2023).
Wakati wenzetu Waturuki wakifanya mgomo wa kutolipwa mishahara kwa miezi 7 sisi tulikuwa na jambo letu kuhusu NSSF lakini tulitulia kwa kuwa tulikuwa katika mazungumzo na uongozi wa Yapi.
Tarehe 27 Agosti 2023 tulikuwa na mazungumzo na HR wa Yapi kuhusu madai hayo ya kutoingiziwa fedha NSSF tangu Desemba 2022.
31 Agosti, 2023 Meneja wa NSSF akaja kukutana na uongozi wa Yapi pamoja na sisi Wafanyakazi tukatoa wawakilishi kwenda kushiriki katika mazungumzo.
Tarehe moja Agosti 2023 tukaenda kwenye kikao kingine na Meneja Mradi akasema baada ya mazungumzo na NSSF wamekubaliana kuwa wataanza kuingiza Tsh. Milioni 400, kisha itafuata Tsh. Milioni 500 na kuendelea kisha kufikia Oktoba 2023 watakuwa wamekamilisha malipo yote.
Malipo hayo tunayoyadai yanahusisha pia wenzetu ambao wameachishwa kazi au walimaliza mikataba yao bila kulipwa.
Kibaya zaidi Lot 1 na 2 miradi inayofanyika hapa inaelekea mwishoni, kuna watu wanatarajiwa kuendelea kupunguzwa kazini kwa kuwa majukumu yanapungua, ukiondoka hapa bila kuwa umejihakikishiwa kuingiziwa chako jua kwamba itakuwa ngumu kupata tena.
Hadi leo (Agosti 28) tunatarajiwa kuingia mwezi wa tisa walichofanya wameingiza malipo ya Desemba 2022 tena kwa baadhi ya Wafanyakazi, wengine hawajaingiziwa.
Tulipowasiliana na NSSF wametuambia kuwa Mkandarasi amekiuka makubaliano ambayo waliafikiana awali.
Hivyo, tunachokiona ni kuwa Mkandarasi anaelekea kutupiga changa la macho, muda wetu wa kufanya kazi unaelekea kupungua na hakuna kinachofanyika, Serikali iingilie kutusaidia kwa kuwa mwajiri kama hataingiza stahiki za Hifadhi ya Jamii hilo ni kosa kisheria.