Wafanyakazi wote 108 wa Ofisi ya Naibu Rais wapewa likizo ya lazima kuanzia mchana wa leo, Oktoba 19, 2024

Wafanyakazi wote 108 wa Ofisi ya Naibu Rais wapewa likizo ya lazima kuanzia mchana wa leo, Oktoba 19, 2024

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wafanyakazi wote wa Ofisi ya Naibu Rais wa Kenya wamepewa likizo ya lazima kuanzia mchana wa Leo 19/10/2024

===
TF-Alert-Share-28-e1729350478384.png

Kwenye taarifa Jumamosi serikali iliamuru jumla ya wafanyakazi 108 katika walioajiriwa mahsusi kumhudumia Bw Gachagua kwenda likizo kutokana na kile kinachotajwa kama “mchakato wa kikatiba unaoathiri naibu rais.”

Walioathirika ni pamoja na maafisa wakuu, washauri na makatibu walioajiriwa kwa kandarasi na mkataba wa kudumu.

Taarifa hiyo iliyotumwa na Katibu wa Usimamizi Patrick Mwangi na nakala yake kutumiwa Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, wengi wa maafisa walioagizwa kuondoka ni wale wa kiwango cha ajira cha T na U.

Wakuu wote wa Idara wameagizwa kuhakikisha agizo hilo limetekelezwa kufikia saa sita adhuhuri Jumamosi, Oktoba 19.

Hatua hiyo ya serikali inaonekana kama inayolenga kutoa nafasi kwa utekelezaji wa mageuzi katika Afisi ya Naibu Rais, Profesa Kithure Kindiki akitarajiwa kushika usukani.

“Wakuu wote wa Idara wanaagizwa kuhakikisha kuwa wameteua, kwa maandishi, afisa atakayesimamia idara zao, na nakala ya barua hizo zitumwe kwa Mkuu wa Wafanyakazi na Katibu Msimamizi,” akasema Bw Mwangi.

Miongoni mwa walioasimamishwa kazi ni aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu ambaye amekuwa akihudumu kama mshauri wa kisiasa wa Bw Gachagua na mbunge wa zamani wa Embakasi Magharibi George Theuri aliyekuwa akihudumu kama mshauri wa kuhusu masuala ya vijana.

Bi Elizabeth Wanjiku, ambaye amekuwa akihudumu katika wadhifa wa Mkuu wa Wafanyakazi katika Afisi ya Naibu Rais pia ni mwathiriwa. Bw Gachagua aliondolewa mamlakani na Bunge la Kitaifa baada ya wabunge 282 kupitisha hoja iliyodhaminiwa na Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse.

Bw Mutuse aliwasilisha mashtaka 11 dhidi ya Bw Gachagua, yakiwemo ukiukaji wa Katiba na utovu wa maadili.

Hata hivyo, Bw Gachagua alikana mashtaka hayo yote na kuwasilisha kesi ya kupinga kuondolewa kwake afisini.

Jaji wa Mahakama Kuu Chacha Mwita ametoa agizo la kusitishwa kwa muda kwa mpango wa kumwapisha Profesa Kindiki hadi Oktoba 24 wakati kesi iliyowasilishwa na Gachagua itakapotajwa mbele ya majaji watatu watakaoteuliwa na Jaji Mkuu Martha Koome.

Aidha, duru zinasema kuwa wafanyakazi wote wa serikali waliokuwa wakihudumu katika boma la Bw Gachagua, Mathira, Nyeri, waliagizwa waondoke Ijumaa asubuhi.

Hatua hiyo ilijiri saa chache baada ya Seneti kuidhinisha hatua ya Bunge la Kitaifa ya kumwondoa afisini, Alhamisi usiku.

Wafanyakazi hao ni pamoja na wapishi na maafisa wa usalama waliokuwa wakilinda boma lake waliagizwa kuondoka mnamo Ijumaa saa kumi na mbili alfajiri magari rasmi ya Bw Gachagua pia yaliondolewa.

Chanzo: Taifa leo

Pia soma: Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua aondolewa madarakani
 
Ruto anachokitafuta atakipata mwaka 2027

Ruto ni dicteta Kama alivyokuwa dicteta Magufuli Hana jipya kwenye siasa za kisasa!!!

Muda ni mwalimu tuendelee kwepo!!!
 
Wafanyakazi wote wa Ofisi ya Naibu Rais wa Kenya wamepewa likizo ya lazima kuanzia mchana wa Leo 19/10/2024

Matunda ya Katiba Mpya
Kenya hakuna katiba bali kuna karatsi inayotumiwa kupata mamlaka kwa kutumia muunganiko wa kikabila.
 
Hawajaachichwa kazi hao, ni likizo tu hiyo maana wanalipwa hela ya likizo na mishahara yao ita flow kwenye B/Acc zao kama kawaida...

Bila shaka serikali ime suspect jambo lisilo la kawaida na kwa hiyo Ili kufanya clearance, imeona ni lazima wafanyakazi wa ofisi hiyo wote watoke kwenye ofisi zao Ili kuruhusu wachunguzi wafanye kazi yao....

Hii ndiyo kawaida na ndivyo inavyotakiwa. Sio sisi hapa Tanzania, polisi wanaotuhumiwa kwa utekaji na mauaji, wahusika wapo tu ofisini na zaidi sana wanajichunguza wenyewe....!!!

Kwa hili la Kenya, haina shaka kabisa kuwa baada ya uchunguzi huo, baadhi, wataenda na impeachment ya Rigathi Gachagua...!!
 
Katiba yao ina changamoto

Unafunga office ya Deputy President kwa sababu ya impeachment ya Mchongo?

Bure Kabisa 😄
 
Katiba yao ina changamoto

Unafunga office ya Deputy President kwa sababu ya impeachment ya Mchongo?

Bure Kabisa 😄
Impeachment ya mchongo..!!???

Hii ni lugha ya wafuasi wa CCM ya Chura Kiziwi wa Kizimkazi...

Bure kabisa wewe Yohana Mbatizaji🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️
 
Impeachment ya mchongo..!!???

Hii ni lugha ya wafuasi wa CCM ya Chura Kiziwi wa Kizimkazi...

Bure kabisa wewe Yohana Mbatizaji🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️
Walichofanya Bunge la Kenya na Seneti ni Kura ya Maoni ya Kutokuwa na Imani na Gachagua binafsi wala haikuwa impeachment ile na ndiyo sababu imekwama

Ni impeachment ya Mchongo kwa sababu Mr Abdul ambaye ndiye mkuu wao wa Takukuru amemclear Gachagua kwamba Ofisi yake haina tuhuma zozote za Gachagua 😂

Hapa Tanzania Kiongozi akizingua analazimishwa Kujiuzulu hakunaga sababu ya utitiri wa Vikao vinavyosheheni Upumbavu mtupu na kujivua nguo🐼
 
1. Kura hiyo ya maoni (unayoiita wewe) ndiyo impeachment yenyewe. Kura ya maoni ni kiswahili na kiingereza chake ni "impeachment"

2. Huyo Mr Abdul na PCCB yake kisheria possibly, hana tuhuma mezani kwake. Lakini kisiasa inakwenda hivyo inavyokwenda...

3. Na kama huna taarifa ni kuwa, Mahakama pia umefanya delayment ya mchakato huo wa impeachment kuwa finalized kwenye senate Ili kumpa haki ya kumsikiliza DP Gachagua. Lakini, mpaka hatua hii, kwa zaidi ya 90% hana possibility ya kupona...

3. Kwa Tanzania kuzingua kwa kiongozi na kulazimishwa kujiuzuru ni pale anapokwenda kinyume na maslahi ya establishment "status quo" na sio kama kina Mwigulu au Bashe ambao wamehujumu uchumi wa nchi kabisa kwenye sakata la uingizaji sukari au kina Masauni, IGP na boss wa TISS kwa kushindwa kulinda uhai wa wananchi kwenye sakata la utekaji na mauaji yanayoendelea..

Kati ya hao kuna aliyelazimishwa kujiuzuru? Hakuna. Kwa sababu matendo yao Yana maslahi kwa CCM na watawala. Wananchi hata kama wananaumia na kufa, serikali ya watawala hawa hawajali chochote Ili mradi miradi yao ya kisiasa Iko salama ingalau kwa kitambo kidogo..
 
Back
Top Bottom