Nadhani hujaeleweka vizuri, mm nahisi unasemea kiwanda cha nguo cha mazava morogoro. Mnalipwa 2,500-3,000/= per day. Ambapo sawa na wale vibarua wa pale viwandani (MeTL-Textiles Ltd) kihonda ambao wanalipwa elfu 3 kwa siku, na wale wanaokuwa sekta ya moto (jikoni) wanalipwa elfu 5 kwa siku. Tatizo la hao wahindi + aboud, ni kwamba wanawadharau sana na kwa bahati mbaya sana; baadhi ya watanzania tuna shida nyingi sana hivyo tunakosa hata nguvu ya kudai haki zetu za msingi kwa kuhofia kukosa hata hicho kidogo. Ngoja wakusaidie wengine, au andika upya post yako ili ieleweke vizuri wenye nguvu wakusaidie mawazo mazuri