Wafuasi wa CHADEMA waliokabiliwa na kesi ya mauaji waachiwa huru Katavi

Wafuasi wa CHADEMA waliokabiliwa na kesi ya mauaji waachiwa huru Katavi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Ocsar Sangu.jpg
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Isengule Mkoani Katavi, Ocsar Sangu na wenzake watano ambao ni wafuasi wa CHADEMA waliokaa mahabusu kwa miaka minne wameachiwa huru baada ya kubainika hawana hatia

Walikuwa wanakabiliwa na tuhuma za kuwaua wafanyabiashara waliokuwa wakinunua mazao katika Kijiji Chao.

Ocsar Sangu ambaye ndiye alikuwa Diwani wa Isengule na wenzake baada ya kuachiwa huru walikimbilia Kanisa Katoliki na kufanya ibada kabla ya kwenda nyumbani kuzungumzia halisi halisi ilivyokuwa mpaka wao kujikuta kwenye mikono ya sheria.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Isaya Kalimwabu amezishukuru mamlaka husika kwa kutenda haki.

Viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Katavi wameendelea kuiomba Serikali kutenda haki na kuweka kando mambo ya siasa na vyombo vya ulinzi na usalama, huku wakisisitiza siasa uwe ni mchezo kipindi Cha uchaguzi.
 
Je hawa kuna remedy yeyote ya kuishitaki serikali for wrong arrest?halafu tunaambiwa sirro ameonekana akiingia nyumba ya ibada!wakati mikono yake imechafuka na damu na mateso ya binadamu wenzake
 
Back
Top Bottom