Elections 2010 Wafuasi wa CHADEMA wazingira ofisi ya Halmashauri Maswa.

Elections 2010 Wafuasi wa CHADEMA wazingira ofisi ya Halmashauri Maswa.

Sokomoko

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2008
Posts
1,915
Reaction score
129
Monday, 01 November 2010

Mamia ya wafuasi Chadema wamaekusanyika katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya ya Maswa wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge katika majimbo ya Maswa Mashariki na Maswa Magharibi.

Mgombea wa Ubunge katika jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chadema, John Shibuda, akiwahutubia wafuasi wa chama hicho, alidai kuwa kuna njama za kumpora kura hivyo kuwataka wananchi kuwa macho.

Msimamizi wa uchaguzi katika majimbo hayo,Elizabeth Kitundu, hajulikani aliko na habari kutoka Maswa zinadai msimamizi hiuyo amekimbia umati wa wananchi hao ambao walionekana kuwa na hamasa ya kutaka kufahamu matokeo.
 
Ukizoea kula nyama ya binadamu utaendelea kula tu alisema Nyerere
 
Hawaoni taabu kuumiza wananchi kwa ajili ya uroho wa ukubwa I hate this politic watu washindane kwa hoja sio kuumiza na kuuana.
 
Huyu mama ndie alikua mkurugenzi na alitumika kumhujumu shibuda tangu kipindi cha kugawa fedha za mfuko wa bunge ambazo ni pesa za mfuko wa jimbo. Alimkatalia kwa nia ya kumhujum na hata pesa za mbunge pia alizikatalia na kumnyima wasaa wa kurudi kwa wananchi kueleza alichofanya


ni huyu huyu ndie alieikomalia tume imuondoe shibuda kugombea... Leo sishangai kuhujumu kura za shibuda. Amedhamiria toka moyoni mwanamke huyu.
 
Back
Top Bottom